University of Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

University of Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ndahani, May 13, 2009.

 1. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Moja ya vitu ambavyo vimefanywa kwa vitendo katika kipindi hiki cha Kwanza cha utawala wa JK ni kuhakikisha kuwa Dodoma University inajengwa na kuanza kuchukua wanafunzi kwa ajiri ya masomo ya juu. Nimesikia inakadiriwa kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi karibu 40,000 kwa wakati mmoja.Litakuwa jambo la manufaa makubwa kama chuo hiki kikiweza kukamilika katika muda na kutoa nafasi ambazo bado zinasumbua za kuwaendeleza watanzania kitaaluma katika fani mbalimbali. Kuna maandalizi yoyote mengine ya kuviwezesha hivi vyuo kuwa na contribution kubwa nchi yetu apart from majengo yanayojengwa? Nini tunaweza kufanya ambacho pengine hatufanyi ili kuviboresha vyuo vyetu viwe vizuri zaidi?
   
 2. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Chuo hiki kimeanza katika hali ngumu sana na ya utisha na kusikitisha.Ukiachilia mbali uhaba wa waalimu ,wanafunzi hawajapata mikopo kwa muda mrefu tangu waanze,Hali inayowafanya waishishi maisha ya omba omba na umalaya kwa wanafunzi wa kike.
  Ni kweli wazo lilikuwa ni zuri saana,Japo halikuwekewa mipango thabiti.Nilibahatika kutembelea mahali pale pakiitwa Chimwaga CCM Complex.Madarasa hayatoshi idadi iliyopo ya wanafunzi.Kwa ujumla maisha ya mwanafunzi ndani ya chuo hiki ni magumu sana.
  Leo nasikia tena kuna mpango wa kuanzisha complex nyingine kubwa sana huko Bagamoyo ambayo imeshapatiwa na wafadhili.Hoja yangu kwanini wasikazanie kukamilisha hicho cha Dodoma kwanza ndipo wafikirie Bagamoyo?
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Uanzishwaji wa vyuo uende sambamba na kuongeza uwezo wa kuajiri ili wamalizapo masomo angalau 60-75% wapate ajira. hivi kuna chombo kinachofanya kazi ya kutafuta uwiano huo? na kama ndivyo kimepata mafanikio gani na kama hakuna mafanikio nini kifanyike?
   
 4. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  BAGAMOYO HUJUI NI KWETU LAZIMA TUACHJE ALAMA. nI KAMA WAKATI Sumaye akiwa PM alianzisha move ya kujenta international airport Arusha akijua wazi kuna Kilimanjaro airport iliyoko jirani kabisa na asifikirie kuijenga kanda ya ziwa yenye rasilimali kubwa
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Uwezo wa kujiajiri ndiyo mwendo wa kisasa.
   
Loading...