[h=2]NAPE ATEMBELEA UDOM LEO, AAGIZA MAJENGO YENYE NYUFA YASHUGHULIKIWE HARAKA[/h] May 24, 2011
CCM imewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ili kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la nyufa zilizoanza kuitokeza kwenye baadhi ya majengo.
Chama kimewaagiza pia viongozi hao kukagua hali ya miundombinu ya majitaka katika maadhi ma maeneo chuoni hapo ili ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inatuamisha maji kutoka katika majengo na kusababisha adha ya harufu mbaya kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazima,m wengine chuoni hapo.
Maagizo hayo yalitolewa leo, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kutembelea chuo hicho na kagua baadhi ya majengo ambapo alishuhudia baadhi ya majengo yakiwa na nyufa.
Majengo yaliyoonyesha kuwa na nyufa ni katiba mabweni ya wanafuzi wa Shule ya Sayansi na Jamii yaliyoko Block 2 na 3 ambapo alionyeshwa na wanafunzi wanaoishi katika mabweni hayo.
"Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yake yanakuwa katika hali bora", alisema Nape.
Nape alionyesha kushangazwa kwake kuona majengo ambayo hayajatimiza miaka mitano tangu kujengwa kwake, kuanza kupata nyufa jambo ambalo alisema ni hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaoishi katika majengo hayo.