Unit za umeme

SALADY

JF-Expert Member
May 8, 2015
220
196
Habarini wana jf.
Bila kuwachosha, naamini wengi wenu au wachache wanaishi kwenye nyumba za kupanga, kila Mara unaambiwa umeme umeisha nimeona leo niwape kidogo elimu ambayo itakusaidia.

Kabla ya kununua chombo kinachotumia umeme unapaswa uangalie mambo yafuatayo.
1. Power angalia lable nyuma ya TV au radio utakuta wameandika = P75W au P150W.
Maana take in kwamba hicho chombo chako kinatumia watts za umeme 75 au 150.
Sasa ili ujue kuwa chombo chako kinatumia unit ngapi unit ngapi za umeme fuatilia hayo mahesabu

E=P*T. Yaan. E= energy
P=power
T=time
Wote huwa tukinunua umeme tunapewa unit kwa kilowatt s hour (kWh).
P/1000*T=kWh
Sasa kama TV au radio INA P75 au P150 chukua hizo 75 au 150 gawanya kwa 1000 utapata na zidisha kwa lisaa limoja utapata, utapata idadi ya unit kwa muda was lisaa limoja, ambapo kama kifaa chako umekiwasha kwa muda was lisaa utapata unit ulizo tumia.

See example below
E =p*t
= 75/1000*1
=0.075kwh
Kwa maana hyo kwa lisaa limoja la
kuangalia TV yako utakua umetumia unit 0.075kwh.

Kumbuka hyo in TV tu kama umewasha na redio,taa na nk unapaswa pia kufanya mahesabu hayo hyo kwa kila kifaa kutegemeana na power yake
 
Aisee..kumbe... vipi matumizi ya water heater....pasi..friji nasikia umeme mwingi huw unatumika..nipe ufafanuzi
 
Aisee..kumbe... vipi matumizi ya water heater....pasi..friji nasikia umeme mwingi huw unatumika..nipe ufafanuzi
Hapo kwenye heater ndio balaa kabisa!!

Kwa kifupi angalia rated power ya heater ..pasi...friji...au majiko ya umeme!! Zinachukua umeme mkubwa sana!
 
Aisee..kumbe... vipi matumizi ya water heater....pasi..friji nasikia umeme mwingi huw unatumika..nipe ufafanuzi
Heater zina kula sana umeme. Unaweza kufa heater ina Watts 3000.

Ki mahesabu,
1kW = 1000Watts

Sasa kama kifaa kina tumia 3000Watts, maana yake ni kuwa Umetumia 3kW. Sasa hii ukizidisha na saa 1. Ina kuwa ni 3kWh ambayo ni sawa na UNIT 3 za umeme.
Na kama kitaa chako kimewaka masaa mawili(2), unazidisha na hizo kW.
I.e 3kW * 2hrs = 6kWh

NB. kW = KiloWatt.
 
Ivi ukitaka kucheki units zilizobaki ni lazima upande kwenye mita uangalie? Au kuna njia ingine??
 
Back
Top Bottom