Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
354
1,340
Wakuu kwema?

JF imefanya mjadala leo kuhusu kupata mbadala wa adhabu ya viboko shuleni, huku lengo kubwa ikiwa adhabu hiyo kuondolewa kabisa shuleni.

Nimesikia watu wanasema bila fimbo wangekuwa wamepotea huku wengine wakigoma kuwa adhabu ya viboko inapaswa kukomeshwa, mimi binafsi naunga mkono viboko kuondolewa, sasa turudi kwenye swali letu la kukaribisha siku ya wafanyakazi kesho;

Je, ungeweza kufika hapo ulipo bila adhabu ya viboko? Sasa umekuwa mtu mzima unafikiri mtoto wako anatakiwa kucharazwa ili mambo yaende? Au atakuja kukushukuru baadaye kama wewe unavyoshukuru kuchapwa leo (kama jibu lako litakuwa hapana).

Twende kazi wakuu.

Pia soma
- News Alert: - Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?
 
Mikwaju si afadhali kuna ngumi,mateke na magongo pia wazee wengine hasira za kukosa hela wanamalizia kwa watoto😂😂
 
Wakuu kwema?

JF imefanya mjadala leo kuhusu kupata mbadala wa adhabu ya viboko shuleni, huku lengo kubwa ikiwa adhabu hiyo kuondolewa kabisa shuleni...
Viboko havina faida.

Kwani thathmini ambayo niliifanyaga niligundua kwamba wanafunzi wanaofanya vizuri darasani sio wale wanaopigwa sana viboko na kuwa watukutu,bali wanafunzi wanaofanya vizuri darasani huwa hawana historia mbovu ya kuwa kwemye mkumbo wa wanaochapwa.

Ila wale ambao watukutu na wanaopigwa sana viboko ndio wanarekodi mbaya madarasani na huwenda hao wakawa ni katika wanafunzi watukutu.

Viboko humfanya mwalimu apate anachokihitaji kutoka kwa mwanafunzi,lakini viboko haviwezi kumsaidia mwanafunzi apate anachokihitaji shuleni.
 
Nikiwa la tano mwaka 92..nilikamatwa navuta sports kichochoroni...shule sijaonekana miezi mbili na napambana niiache kabisa..aisee nilipigwa kama mmbwa mwizi... nilichangiwa na ofisi yote.

Kuna buku niliiba ya mia mbili mia mbili zile za noti kubwa (mia mbili za noti zilikua za aina mbili ndogo na kubwa) aisee acheni nilipigwa na maza kakaa pembeni wakichoka ananikamata.

Nilibadilika mno aisee..
 
Viboko havina faida.

Kwani thathmini ambayo niliifanyaga niligundua kwamba wanafunzi wanaofanya vizuri darasani sio wale wanaopigwa sana viboko na kuwa watukutu,bali wanafunzi wanaofanya vizuri darasani huwa hawana historia mbovu ya kuwa kwemye mkumbo wa wanaochapwa...
Samahan, we umesoma primary school au shule ya msingi?
 
Samahan,,,we umesoma primary school au shule ya msingi?
Nimesoma shule ya msingi ya kata.

Nimesoma shule ya sekondari ya kata.

Na shule zote hizo zilikuwa na viboko.

Binafsi nimeshapigwa sana viboko ila sikuona msaada wake zaidi ya kunizidishia uwoga darasani na kuninyima uelewa wa kile ninachofundishwa.
 
Nimesoma shule ya msingi ya kata.

Nimesoma shule ya sekondari ya kata.

Na shule zote hizo zilikuwa na viboko.

Binafsi nimeshapigwa sana viboko ila sikuona msaada wake zaidi ya kunizidishia uwoga darasani na kuninyima uelewa wa kile ninachofundishwa.
Kwasisi,,,,tulio soma shule ya msingi "mwalimu mpole Huwa hapendwi na wanafunzi"
 
Nikiwa la tano mwaka 92..nilikamatwa navuta sports kichochoroni...shule sijaonekana miezi mbili na napambana niiache kabisa..aisee nilipigwa kama mmbwa mwizi... nilichangiwa na ofisi yote..
Kuna buku niliiba ya mia mbili mia mbili zile za noti kubwa (mia mbili za noti zilikua za aina mbili ndogo na kubwa) aisee acheni nilipigwa na maza kakaa pembeni wakichoka ananikamata...!
Nilibadilika mno aisee..
Kwa maana hiyo bila kupigwa usingebadirika?
 
Back
Top Bottom