Ungelifanyaje? Mchana kweupe, ukiwa na gari lako kwa mwendo si wa kasi sana, mitaa ya sayansi anakupiga mkono binti. Unajiuliza ni nini? Unataka kupitiliza lakini hisani inakujia na kuamua kusimama. Anakusarimu binti mzuri tu, anakuomba samahani kwa kukusimamisha kisha anakuambia anaomba lifti kama unaelekea posta umsaidie. Unamwambia mimi naelekea maeneo ya agakhani, sifiki posta. Anakwambia basi nisogeze hata mbele utakuwa umenisaidia. Unamchukua, bila kumsemesha chochote kuhusu mapenzi isipokuwa maongezi tu ya kawaida.
Unafika karibu na unakoelekea unamwambia, kwa kuwa mi naelekea kushoto basi nikuache hapa. Mara unasikia, umwache nani? ndo utanijua mi nani, nilipe elfu hamsini yangu, kama haunilipi napiga kelele. Na muda huo sauti anayotumia ni ya juu tayari tena ya hamaki. Ungelikuwa wewe ungelifanya nini?