Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,202
- 2,035
Habari zenu ndugu.Tukiwa tunaokaribisha mwezi wa ramadhani ni vizuri kutakiana mfungo mwema na Allah atufanyie wepesi katika funga zetu.
Ni hivi ni kama wiki tatu tangu tumefiwa na mfanyakazi mwenzetu.Huyu mfanyakazi mwenzetu tuliishi nae vizuri hapa kazini hivyo baada ya kiso chake ofisi iliamuwa kurudisha kwao mwili wa marehemu,kwao ni Sumbawanga.Kama ilivyoada ikabidi kazini watoke japo wafanyakazi kadhaa ili kupeleka msiba,tunashukuru kwani wenzetu wawili walikubali kwenda na msiba Sumbawanga.katika msafara huo kuna dereva,Mwanamke 1 na mwanaume 1 pamoja na mwili wa marehemu.Yapata wiki tatu sasa tangu waende msibani ila wakati wa kurudi gari lao Limepata matatizo hivyo ni ngumu kurudi nyumbani kwao.
MSAADA WENYEWE NI HAPA...
Yule Mwanamke ni mke wa mtu na mme wake tunafanya kazi ofisi moja.Sasa Mme wake hana furaha kabisa tangu kuondoka kwa mke wake alafu kingine hana amani juu ya mazingira aliyopo mke wake na huyo mwanamme.Kila anapojaribu kumwambia mkewe arudi mke hataki anasema hawezi kurudi na kuwaacha wenzake katika mazingira hayo.Sasa akaja kuniomba ushauri mi nikamwambia mfuate huko huko alipo,je nimekosea kumpa ushauri huo?kama ungekuwa wewe ungeshauri nini
Karibuni kwa mawazo yenu