palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,463
Yapata miaka 15 iliyopita bwana mmoja dar ilipata kuoa.. Mwaka wa kwanza ukaisha kugegedena kukaendelea bila mafanikio yoyote ya kupata mtoto. katika desturi zetu za kiafrika ongea vyote lakini ndoa bila mtoto masimango hayaishi. Wanandoa hawa hawakukata tamaa, ikawa mwaka wa pili, tatu..mpaka mwaka wa kumi unafika hakuna dalili zozote. Mwanaume kipindi hichi ni mtu maarufu kutokana cheo chake na anachekwa na marafiki zake kuwa umeshindwa hata kutoka nje ya ndoa ukapata hata kamoja? Jamaa achakua ushauri na kuufanyia kazi lakini alikuwa mwangalifu kuhakikisha anapata mke wa mtu au dada ambaye tayari alishazaa. Katika mihangaiko yake akakutana na dada mmoja akaanzisha mahusiano wakati huo dada akidai yeye ana mtoto nyumbani na ameolewa ingawa mume wake kazi zake ni za kuondoka asubuhi kurudi jioni hivi kuchepuka itakuwa rahisi zaidi.
Wakaanza kuvinjari naye kama mchepuko wake wa kudumu huku jamaaa akitoa matumizi ya kufa mtu. Huyu dada yeye ni mwenyeji wa tanga na wakati wamekutana na mume wanayeishi naye hadi kupata mtoto hawajawahi kwenda tanga kuwaona ndugu wa mke. Siku moja mchana aligegedana na mchepuko wake na usiku kama kawa na mumewe nyambani. Mwezi uliofuata hakupata siku zake na kumwambia mumewe kuwa ana mimba. Mume akafurahi sana. Wakati huohuo mchepuko wake nao ulitaka kujua maendeleo, nao ukajulishwa mimba imetiki. Mume na mchepuko wakaendelea kulea mimba mpaka mke anajifungua mtoto wa kiume. Mke kipindi hiki bado hajui hasa mtoto ni wa nani. Mchepuko ukaendelea kutoa matunzo kama kawa bila mume kujua nini kinaendelea. Wakati mtoto amefikisha miaka miwili mchepuko ukataka kujiridhisha kuwa pesa yake inaendelea kulea mtoto wake na si vingininevyo. Hii ilikuwa mwaka 2010 wakati mchepuko unataka ifanyike "DNA pertainity test". Mke alisita lakini hakuwa na jinsi mipango ilifanyika kwa siri kubwa na hatimaye wakatinga kwa mkemia mkuu na kuchukuliwa sampuli. Baada ya kama wiki 2 hivi wakaitwa kwa ajili ya majibu. Majibu yalikuwa "Based on the DNA analysis the alleged farther , mchepuko is not excluded as the biological farther of the child X because they share the same genetic markers by 99.9999%". Kwa maneno mengine ni mchepuko ndiye baba halisi wa kibaolojia kwa 99.9999% na si mume wa nyumbani.
Mchepuko meno yote 32 nje maana hakuwahi kujaliwa kupata mtoto katika maisha yake yote. Lakini kwa upande wa mke supu ikawa imetiwa nazi, sasa atafanyaje kutatua hili tatizo. Mchepuko ukadai kwa kuwa yeye ndiye baba halasi hivyo anapaswa kuchukua mtoto na kurudi naye kwake. Mke akachanganyikwa sasa mumewe akirudi jioni atamwambia nini kuhusu mtoto, moto utawaka. Mke akashauri kuwa kwa kuwa wao tayari ni wazazi lazima waaminiane na wapange nini cha kufanya lakini mtoto kwa siku hiyo lazima arudi nyumbani naye. Wakakubaliana mke apange safari kwenda tanga na mumewe akimpa ruhusa basi hapo ndipo atamkabidhi mtoto huku mume akijua mke na watoto wote wawili wameenda tanga. Safari ikaiva mume akaondoka kwenda kwenye mihangaiko asubuhi na mke kwenda tanga majira ya saa nne asubuhi. alipofika ubungo mchepuko ukaja ukapewa mtoto na mke akamtumia sms mume kuwa kuhusu mtoto na kuwa tayari alishakwisha kumkabidhi mchepuko. Mume akachanganyikwa asijue la kufanya kwa vile hajawahi kufika kwao tanga na hajui wapi pa kuanzia. mke hakwenda tanga alitafuta sehemu nyingine dar na kupanga ili andelee na kuishi. Mume bado anasisitiza mkewe arudi home na yeye amemsamehe waendelee kuishi pamoja kwa vile yeye bado anampenda lakini mwanamke bado haamini maana mume anaweza kumfanyia kitu kibaya.
Ungekuwa wewe mwanamke ungerudi kwa mume undelee kuishi naye?