Tarime one
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 2,246
- 1,742
mume huwezi stukia kama huwa unaacha pesa ya kutosha kuzidi matumizi ya nyumbani. Hapo hela ya mchepuko ilikuwa inatumika kivingine, unajua mara nyingi katika ndoa pesa anayoiingiza mwanamke mara nyingi mwanamke huitumia kwa mahitaji yake binafsi.
Hii ilishatokea kwa jirani yetu mmoja ambaye alikuwa na fedha nyingi na alikuwa anamuachia mkewe fedha nyingi sana za matumizi, mkewe alikuwa anaishi kama malkia. Pamoja na hayo mume aliambulia kulea second born ambaye sio wake, na alistukia baada ya kuzaa mtoto wa tatu. Mtoto wa pili alikuwa hafanani kabisa nae, lakini aliamua kuuchuna kwa sababu alikuwa anamuamini mkewe hivyo hakusema neno lolote. Mume alikuwa ni mkurya mweusi kama jaluo, mke alikuwa wa-tanga nae alikuwa mweusi wa kawaida, mtoto alikuwa mweupe sana.
Bahati mbaya siku moja Mume karudi ghafla nyumbani kakuta mke yuko na muuza urembo na kapu lake, muuza urembo alikuwa amefanana kupita kiasi na mtoto wao wa pili, mume alistuka sana akaropoka huyu ndie babayake fulani(2nd-born), mume aliishiwa nguvu hata hakuweza kuleta fujo, muuza urembo akaondoka zake.
Huyo alikua mkurya feki sio wale wenyewe.