Ungekuwa Rais Samia nani ungeanza kumtimua?

Ungekuwa Rais Samia nani ungeanza kumtimua?

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,707
Hakuna ubishi Rais Samia Suluhu Hassan angependa awe na timu yake itakayomwezesha kutawala bila hofu hadi muhula aliorithi uishe.

Hivyo, wapi wengi watakaoangukiwa na shoka lake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba.

Mie ningependekeza aanze na Dk Bashiru Ally Kakurwa ambaye alikaririwa akisema kuwa asingekubali kuteuliwa cheo chochote au kugombea baada ya kuteuliwa Katibu Mkuu wa CCM.

Je, wewe unasemaje?
 
DC wa Hai, Ole Sabaya
RC wa Mbeya, Chalamila
Waziri wa Tamisemi, Jaffo

Hawa watu watatu walichojua wao ni kumwabudu na kumtukuza "yesu" wao hayati Magufuli, badala ya kuwatumikia wananchi wa nchi hii ambao kutokana na kodi zao ndiyo wanalipwa mishahara yao
 
Halafu huyo Bashiru akiondolewa kwa hizo sababu ulizotaja, wewe kama wewe, itakusaidia nini na familia yako kamanda? [emoji16][emoji16][emoji16]
Itanisaidia kwa kujenga utamaduni wa watumishi wa umma kuwajibika kwa matamshi yao ambayo pia itawasaidia watu kama wewe na yeye binafsi ukiachia mbali rais na taifa. Umeelewa mwanangu?
 
Acha chuki za kuwaombea mabaya wenzio. Chapa kazi ongeza kipato acha majungu.
Maskini mwanangu usiyejua mambo. Pole sana. Ally alisema mwenyewe kuwa asingekubali kuteuliwa cheo chochote baada ya Ukatibu Mkuu wa CCM. Hayo ni maapizo na maneno yake ninayomkumbusha ayakumbuke na kuyafanyia kazi kama mtumishi wa umma.
 
Hakuna ubishi. Rais Samia Suluhu Hassan angependa awe na timu yake itakayomwezesha kutawala bila hofu hadi muhula aliorithi uishe. Hivyo, wap wengi watakaoangukuwa na shoka lake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba. Mie ningependekeza aanze na Dk Bashiru Ally Kakulwa ambaye alikaririwa akisema kuwa asingekubali kuteuliwa cheo chochote au kugombea baada ya kuteuliwa Katibu Mkuu wa CCM. Je wewe unasemaje?
Kwanza ningemhakikishia CDF kuwa cheo chake anaendelea nacho.

Pili ningefukuzilia mbali haya mataka taka.
  • Bashiru
  • Doto wa hazina
  • Mwigulu
  • Wakuu wa mikoa wote kasoro yule wa Geita.
  • Huyu Katelefoni
 
Kama ulivyotenda nawe ndivyo utavyotendewa.

Unaweza kushangaa yule usiyemtegemea kutumbuliwa ndiye akawa wa kwanza kutumbuliwa, lakini ukifatilia kwa undani wake waweza kuta alimfanyia fitna hata mama asifanye vema kwenye u VP wake.
Hii kitu ipo sana tu na tuwe na subira.
 
Hakuna ubishi. Rais Samia Suluhu Hassan angependa awe na timu yake itakayomwezesha kutawala bila hofu hadi muhula aliorithi uishe. Hivyo, wap wengi watakaoangukuwa na shoka lake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba. Mie ningependekeza aanze na Dk Bashiru Ally Kakulwa ambaye alikaririwa akisema kuwa asingekubali kuteuliwa cheo chochote au kugombea baada ya kuteuliwa Katibu Mkuu wa CCM. Je wewe unasemaje?
Aanze na Wizara ya afya
 
Kumbe unapenda tumbuatumbua za kionevu? Samia Hana Ujinga Kama wako. Atafuata nyayo za JPM kutumbua wazembe na wabadhirifu wa Mali za umma.
 
Kabla ya Kuwa Rais alikua Makamu wa Rais angeanzia ofisi yake ya Zamani ambayo Kuna mtu ananyanyasa sana watumishi na mama anamjua vizuri sana apige yule mtu pale
 
Sasa ni wakati wa kusimama na Mh Rais JMT.
Na mshauri amuondoe mtu kwasababu za haki na kweli. Hawezi kujitenga na utawala wa JPM maana yeye alikuwa sehemu yake na msaidizi no1.

Akisikiliza ushauri wa aina hii ya mleta uzi atajikuta ana maadui wengi kuliko wanao msupport. Ni kama muonekano wa ulinzi wake jana Chato. Hauna tofauti na muonekano wa ulinzi wa Diamond msanii. Rais ni mamlaka inayotakiwa kuwa na muonekano wa kutia utiisho kwa unao waongoza. Ukisha kuwa na ulinzi wenye muonekano sawa na Diamond utiisho wa mamlaka ukowapi?

Tuone wale jamaa wenye mabunduki mzitomzito wakiendelea kumlinda Mh Rais Wetu. Magari yenye miantena mingi mingi hata kama antenae ni za matoyi. Tusipunguze ajira tuongeze.
 
Back
Top Bottom