Undumilakuwili wa Mbowe na mustakabali wa Chadema

mkukurukaji

New Member
Jul 29, 2017
4
5
Katika chaguzi ndogo zilizopita Mbowe na Chadema yake waliwahi kujitoa kushiriki katika uchaguzi mdogo na uliofuata walirejea tena na kushiriki uchaguzi wa Buyungu na juzi wa Ukonga na Monduli.

Wakati alipotangaza kususia alitoa madai kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki na kuwabebesha mzigo nec na wasimamizi wa uchaguzi lakini, walijitafakari wakarejea tena kwenye uchaguzi bila kutuambia waliamua kurudi kwenye chaguzi kwa sababu zipi wakati alishazitia doa nec na wasimamizi.

Leo Mbowe ametutangazia kwamba Chadema kinajitoa kushiriki chaguzi ndogo zijazo, mbona Mbowe anakuwa Ndumilakuwili, leo anatutangazia hivi kesho unarudi kulekule ulikokuwa.Kama hoja ni kujenga chama mzee wetu chama kinaimarika kwa kupambana kwenye chaguzi sio kula ruzuku tu.

Demokrasia ya nchi haikuzwi kwa kususia au kama chama chako kinajinadi kuwa ni chama cha demokrasia kinatetea demokrasia gani zaidi ya hii ya kupambana kwenye chaguzi.
 
undumilakuwili wa Mbowe ni kutokukubali buy out clause ili aiangamize CDM isahaulike. Hakuna anayefurahia hili jambo.
 
Katika chaguzi ndogo zilizopita Mbowe na Chadema yake waliwahi kujitoa kushiriki katika uchaguzi mdogo na uliofuata walirejea tena na kushiriki uchaguzi wa Buyungu na juzi wa Ukonga na Monduli.

Wakati alipotangaza kususia alitoa madai kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki na kuwabebesha mzigo nec na wasimamizi wa uchaguzi lakini, walijitafakari wakarejea tena kwenye uchaguzi bila kutuambia waliamua kurudi kwenye chaguzi kwa sababu zipi wakati alishazitia doa nec na wasimamizi.

Leo Mbowe ametutangazia kwamba Chadema kinajitoa kushiriki chaguzi ndogo zijazo, mbona Mbowe anakuwa Ndumilakuwili, leo anatutangazia hivi kesho unarudi kulekule ulikokuwa.Kama hoja ni kujenga chama mzee wetu chama kinaimarika kwa kupambana kwenye chaguzi sio kula ruzuku tu.

Demokrasia ya nchi haikuzwi kwa kususia au kama chama chako kinajinadi kuwa ni chama cha demokrasia kinatetea demokrasia gani zaidi ya hii ya kupambana kwenye chaguzi.
Ningewaelewa zaidi kama wangesusa chaguzi zote
 
Back
Top Bottom