Understanding the Domain name System (DNS) and Domain names

tzhosts

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
378
467
Je unajua kwamba domain name ni mtaji?

Unapoona jina kama jamiiforums.com hii ni domain name unapoona jina kama tzhosts.com hii ni domain name.Leo nataka tuzungumzie kidogo maana na umuhimu wa domain na jinsi ambavyo unaweza kuitumia ili kujiongezea pesa.

Ngoja niwape mfano.Leo hii unaweza kuamua kusajiri jamiiforums.co.tz kama bado ipo na ukaamua kuweka maudhui ambayo hayahusiana na jamii forum.Kwa hakika utajikuta Maxence Melo anataka kuinunua kutoka kwako kwa gharama yoyte ili tu alinde brand yake.Hio ndio thamani ya domain name.Ni BRAND.

Domain name ni jina ambalo linasomwa na wanadamu na kuwaunganisha na anuani ya IP ya website husika.Anuani ya IP ni anuani ya Mashine/Compyuta ambamo maudhui ya website husika yamehifadhiwa.Kwa mfano server za JF zin anuani yake ya IP na server za tzhosts.com nazo zina anuani yake ya IP.Anuani ya IP huwa ni namba mfano 127.0.0. Kama ungetakiwa kutumia hizi nama kwa ajili ya kufikia website basi ingetakiwa ujue namba za websites zaote huku duniani,kwa kweli ingekuwa ni kazi pevu sana.Ndio maana Domain name system ikatengenezwa ili kurahisisha mchakato huu.

Domain name system inahusika na usimamizi wa DNS records ambazo ziko za aina nyingi kama vile NS,A,AAA,CNAME,MX,TXT ambazo kimsingi kila moja ina kazi au jukumu lake kulingana na mahitaji yake.

Kwa mfano.unaona kwamba website inaweza andikwa kama tzhosts.com basi ili kuhakikisha kwamba maudhui yako yanapatikana katika links zote unaweka maelekezo kwenye DNS records ili kuweza kuhakikisha maudhui yanaonekana kote.Unapofahamu kutumia DNS vizuri unaweza kuioa tovuti yako nguvu zaidi na uwezo zaidi na inaweza kuwa na matumizi zaidi.

Ukienda kwa watu wanaohusika na usajili wa domain names za .tz watakuuliza iwapo tayari una DNS server yaani server maalum kwa ajili ya kusajili na kuelekeza domains, kama unayo basi watakuwa tayari kukupa nafasi ya kuwa muuzaji wa domain names.DNS server inakuwa na uwezo wa kusadifisha domain names.

Je unahitaji mfumo wa kusimamia Biashara yako?Website,n.k.?Je unahitaji mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara ya TECH kwa mfano kuwa muuzaji wa domain names,website na digital products?Kama jibu ni ndio wasiliana nasi kwa email: info@tzhosts.com
 
Hii kitu nimesikia muda mrefu sana hapa bongo mambo ya tech yapo nyuma sana sana kuna wahindi tayari wana Domain za TZ Wamezifanya sasa ukitaka hilo jina inabidi ununue kwa yule alilolifanya lile jina juzi kati nilingalia DOMAIN NAMES nilipata kiwewe kila ninaloandika lipo.
 
Back
Top Bottom