Undani wa John Mnyika na John Heche

Hii nimeipenda zaidi....Hakuna kitu kikubwa katika maisha ya kijamii kama HESHIMA na UTII...

"Utii pasipo uhuru ni Utumwa. Na Uhuru pasipo Nidhamu ni Wendawazimu" J. K. Nyerere.
Ni angalizo tu mkuu!
Mungu wetu anaita!
 
"Utii pasipo uhuru ni Utumwa. Na Uhuru pasipo Nidhamu ni Wendawazimu" J. K. Nyerere.
Ni angalizo tu mkuu!
Mungu wetu anaita!

Mkuu,
Nakubaliana na wewe, lakini kwa maoni yako unadhani Utii uambatane na Mipaka? Msingi wa yote haya ni ile tabia ya vijana kutofautiana na viongozi wao na badala ya kupingana nao kwa hoja na kwenye vikao, wanakimbilia JF na FB kwa ID zao halisi au batili na kuanza kuwatukana viongozi wao. Tena matusi kabisa na kuwadhihaki na kuanza kujadili maisha yao binafsi...
 

Mkuu wangu nimefurahi sana ulivyomjibu.
Unajua kitakachowaangamiza vijana wengi katika siasa ni kukosa subira na kutaka mafanikio kwa haraka haraka.Wanapokosa wanapata ghadhabu wanachanganyikiwa na kuangalia namna ya kuondoa stress zao.Sasa wanadhani kuondoa Stress ni kutukana viongozi matusi ya nguoni.Wakichoka kutukana matusi wanaanza kujadili maisha binafsi ya wenzao.
Ni wazi kwa mwendo huo vijana wa namna hiyo hawatafika.Watadhani watakimbilia vyama vingine au kuanzisha vyama lakini nawahakikishia watasambaratika kwa sababu hawataweza kukaa pamoja kwa tabia za namna hiyo.
Vujana wanapaswa kujifunza kitu kimoja,mafanikio waliyo nayo viongozi wakuu wa CDM Dr Slaa na Mbowe ni kutokana na uvumilivu wao wa kisiasa vinginevyo nao wangekuwa tu historia leo.

Vijana wanapaswa kubadilika sasa wakitaka mafanikio ya mbeleni.
 

Mkuu japo umenidhania, lakini nikwambie tu, ulichosema hapo juu ndio lengo kuu la mifumo ya kudandia ovyoo ovyoo(Demokrasia)! Na usiseme vijana tu, utakuwa unaukimbia Ukweli, ni asilimia kubwa ya watu walio kwenye vyama, si wazee wala vijana, wote sawa tu!
Demokrasia ni Ushindani wa Hoja juu ya Sera na Falsafa! Ndivyo ilivyo kwa wenzetu(nje), kinachofanya waweze hilo ni "Condunssive Envirnment for Critical Thinking/Reasoning", anapokea hoja ya mtu critically, anaimeng'enya critically, mwisho anaijibu critically, aidha kwa kuipinga ama kukubaliana nayo! Ni mazingira yao yameruhusu wao kuwa hivyo! Naposema Mazingira yao namaanisha kila kitu chao, kuanzia uchumi, siasa na utamaduni wao!
MAZINGIRA HAYO HAYAPO KWETU! Mazingira yetu hayaruhusu TAFAKARI ZA KINA, ukianzia Kiuchumi, kisiasa na kitamaduni. Mfano mdogo tu: Mavyuoni, "mwanafunzi amecheleshewa posho yake kwa wiki zaidi ya 3, mama yake nyumbani mgonjwa anatarajia pesa hiyo kidogo akatibiwe(tu watoto wa mkulima), mkufunzi ametoa vitini asiyekuwa nacho haingii kwenye mtihani" mwanafunzi huyo anapoenda kuhoji, eti anajibiwa "kuwa mvumilivu tupe muda kidogo, c unajua hili na lile", akipata ghadhabu na kutukana ni kosa? Demokrasia inasema NDIO, nanyi ndiooooooo! Mama yake kesho anakufa, bado unataka ATII! Ni Wendawazimu! Mazingira yetu hayaruhusu siasa za kuvumiliana, tusingeivumilia CCM, labda leo mama wa huyu mwanafunzi angekuwa anasherehekea kuhitimu kwa mwanae!
UTII LAZIMA UWE NA MIPAKA! Haijalishi ni kwa nani, hata kwa baba na mama yako! Kuna jambo moja tu ambalo huwa halina mipaka, nalo ni MANTIKI! Halifungwi na chochote, hata damu ya mtu!
UTII kama UHURU, ni lazima uwe na MIPAKA ndugu SEBM!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Ovyooo.hawa jamaa unaowasifia ni ovyo sana,kwanza sifa ya kiongozi mzuri anatakiwa awe intelligent,na msimamizi mzuri wa hoja.
Heche ni mtupu kichwan kasoma SAUT kwa kuungunga sana mpaka kumaliza,kama ndo hazina za cdm basi cdm nayo ni hoi kwelikweli.
 

Hawa ndiyo wale watu wanaojishushia heshima na kuonekana watupu kichwani.
Mtu kaleta hoja yake wewe badala ya kujadili na kutoa hoja zenye mashiko unaleta mambo ya taarabu.Mmejikita kwa chuki binafsi bila sababu yoyote.
Kwa nini usisome tu na kukaa kimya kuliko kujidhalilisha?
 

Ben hata mimi nampongeza sana mkuu kwa kushinda hiyo vita ya kuunganishwa na kina Habibu Mchange na Mwampamba, Huyu jamaa amedhihirisha usomi wake kwamba ni wa maana na Huyu jamaa ni lulu kwa taifa siyo tu kwa chama wakuu
 
hakuna chama cha siasa duniani chenye focus ya kufanya kazi za utekelezaji wakati hakikusanyi kodi wala hakina vyanzo vya mapato vya kiserikali ni vyema ukatumia muda wako kutafakari kuwa je ni kweli CHADEMA wanachokosoa ni kweli ama si kweli! na pia nilitarajia wewe ukazungumzia nini ambacho serikali imefanikiwa wakati chadema ikilalamika kudai haki si kulalamika utambue hilo kuikosoa serikali ni jukumu la kwanza la chadema utambue hilo pia
 
inteligent ni mulugo sio pale southern hill alikuwa haungi kitu kwani heche saut alisoma miaka mingapi alipata G.P.A ya ngapi?
 
Mkuu mie sina hata la kuongeza kutokana na hii kitu yako ni kwamba nakubaliana na yote uliyoyasema kwa 100% hawa vijana wanatisha kwa anga za siasa tanzania just cheki umri wao lakini wanawapelekesha watu wenye umri mara tatu ya umri wao bila kuogopa na sio kwa kuwatukana bali kwa hoja zilizoenda shule kwani hata Pinda alikiri mwenyewe.
 

ngoja nikajiandikishe maana nimeguswa na maneno ya mtumishi muongo moja umepita bila kupiga kura yani tangu uchaguzi wa mwaka 2005 nilitakiwa kujiandikisha ila nimetambua kwamba nimefanya makosa mbele ya Mungu na wanadamu kutotizmiza haki yangu ya msingi kumchagua kiongozi nimpendae tehe teh
 
mkuu tuntemeke swala la CHASO ni muhimu kwa ajili ya kuvuna vijana wapigania mabadiliko ya kweli hapo nakuunga mkono
lakini huyu binti yetu SHONZA ameamua mwenyewe na wote tunamwona akijiandaa kusumbua baraza lao labda tumfanyie maombezi aepukane na siasa za shibuda
 
kwani lazima uwe na masters ndo ujue/uweze uongozi? Umewasaau prof:j.magembe,
 

Hapo ndipo napoanza kuamini wote ni wababaishaji tu si chama kilichoko madarakani wala vyama vya upinzani, Kama hakuna chama cha upinzani kitakachothubutu kuonyesha njia kwa vitendo,vitakuwa na umaarufu lakini haviwezi kuaminika kwa wanyonge hata siku moja, siwezi kushawishika kwamba CDM hawana uwezo wa kuonyesha utendaji kwa kuchagua mambo muhimu yanayowagusa wanyonge waliowengi na kuwasaidia, eti mpaka wasubiri waingie Ikulu wakusanye Kodi, haya ni mawazo ya Utopia!! UNAPOKUTANA NA MTU ANALIA KWA USTAARABU TU WA KAWAIDA KABISA UNATOA KITAMBAA CHAKO CHA MFUKONI UNAMPATIA AFUTE MACHOZI.." sio unamsaidia kulia.

Kwa kiwango chochote wanachopata CDM ikiwa ni ruzuku, misaada kutoka kwa chama rafiki,michango ya wanachama,harambee, michango ya wabunge na "fundrising" yote hiyo wanapaswa waanze taratibu kuchagua mambo muhimu wasaidie wananchi, wanajiandaaje kuongoza nchi hawajui kuwahudumia wananchi? Napata taabu sana kutahmini ikiwa kuna watu makini Tanzania wenye nia ya dhati na utashi wa kuwatumikia watanzania ikiwa kuna watu bado wana fikra kama zako!!

Kitendo cha kuwa shupavu na mahiri katika kulalamika na kueleza udhaifu wa chama, serikali ama mtu mwingine sio dalili ya kuwa na nia safi ama utashi wa kuwatumikia watanzania, tutahitaji tujiridhishe kwa historia yako katika kuwasaidia watanzania,na watanzania wa leo wamechoka kusikia Blah....blah....blah! ikiwa watanzania wamekata tamaa basi wewe uanayejinasibu kuwa mkombozi wao utembee katika maneno yako!! ''SIO KUHUBIRI MAJI KISHA WEWE UNAKUNYWA MAZIWA'' ni unafiki mkubwa na kamwe huwezi kuaminika hata kidogo.
 

Mkuu Shibalanga
Ingawa umechangia kwa jazba sana lakini ninaamini mchango wako umeongeza thamani ya andishi langu.
Nina hakika viongozi mbalimbali wa CDM wanapitia mada hii kila mara kupata mawazo ya kujenga.
 
kwani lazima uwe na masters ndo ujue/uweze uongozi? Umewasaau prof:j.magembe,

Mkuu ruhi
Inasikitisha sana kuona mpaka leo watu wanaamini kusoma sana ndiyo kigezo cha uongozi.
Wapo watu waliosoma sana lakini wameharibu sana kwenye nafasi zao na wapo wasiosoma sana ama wenye elimu ya wastani lakini wamefanya makubwa.
Mifano ipo mingi sana sina hata haja ya kuitaja.
 
Umesahau kuwa mnyika ana maumivu ya kichwa ya mara kwa mara, jee na heche pia?
 

Mkuu kiribo

Niseme kidogo kuhusu huyu Binti Shonza,huyu binti ni mzuri sana kiuongozi kwani namfahamu vyema tangu akiwa mwaka wa kwanza chuoni.
Tatizo lake moja tu ni kudanganywa na akadanganyika.

Unajua nilisoma siku moja makala ya Dr Kitila niliipenda sana.Dr Kitila alisema hawa vijana wanapochaguliwa nafasi za uongozi wanapaswa kupata semina za maadili ya uongozi.Wanapaswa kujua miiko ya Uongozi.

Sasa kitendo cha Shonza kwenda kwenye vyombo vya habari kumpinga Mkiti wake ilikuwa ni mbaya sana kwake.Na hii itamgharimu Shonza kisiasa maisha yake yote.

Kwa ninavyomjua Shonza naamini kuna vijana walimuingiza kwenye mtego naye akaingia mkenge.Ni vigumu sana viongozi wenzake kumuamini kwa sasa.Kwani kulikuwa na hasara gani Shonza kusubiri vikao ndipo amshambulie Mkiti wake?

Ujana bwana maji ya moto usipokuwa makini utaungua.Hata hivyo naamini Shonza amejifunza kitu.
 

Comrade Smallvile
Kwanza hongera kwa kuchukua hatua baada ya kusoma mada yangu.

Nimekuwa nikisisitiza siku zote umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura.Ndiyo maana nasema hawa akina John Mnyika,John Heche,Ben Saanane na vijana wenzao wanapaswa kujua bado wana kazi kubwa kusambaza elimu ya Uraia vijijini.Wajichimbie vijijini kuliko na idadi kubwa ya watu.

Binafsi sioni haja wala maana yoyote pale Dr Slaa anapolakiwa na msururu wa gari mia mbili na kuhutubia watu mpaka elfu kumi huko mikoani,lakini uchaguzi unapokuja chama kinapata kura chache.Bila wananchi kuelezwa umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura itakuwa kazi bure.

Kina Mnyika,Heche,Saanane na wenzao wanapaswa kulipa hili umuhimu mkubwa.
 

Mkuu Mboko

Asante sana kwa kukubali andiko langu.Nisema tu kwamba vijana hawa wanapaswa pia kupokea pongezi zako kama changamoto kwao ili wasonge mbele zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…