Nimejaribu kulima kama eka 2 lakini kama layman kwani sikufanya utafiti wa kina na nimelimia kilomita kama 300 magharibi ya Dar.Habari zenu wana JF. Kupita kwangu kwenye hii forum ya biashara na uchumi kumenipatia mimi muamko mkubwa wa kuanxa kufanya biashara pia, hivyo nawashukuru watu mbali mbali ambao wamekua wakiandika na kuchangia mambo makubwa humu ndani.
Kutokana na huu muamko, nimedhamilia kujikita kwenye ulimaji wa tikiti maji lakini sina mwanga mkubwa kuhusu hili zao kwa mfano:
1. Ni aina gani ya tikiti nzuri?
2. Kuanza inahitaji shilingi ngapi, ukijumlisha na mbegu na fertilisers na malipo ya wafanya kazi? (chukulia kwa ekari moja)
3. Je ukiwa unapanda ni nafasi gani unaacha shimo hadi shimo?
4. Je ekari moja inaweza kutoa matikiti kama mangapi takribani?
5. Faida (gross profit) inayoweza kupatikana kwenye ekari moja.
6. Gharama za uendeshaji wa shamba ni kama shillingi ngapi?
Ningependa nifahamishwe hivyo vitu
ASANTENI
Nimejaribu kulima kama eka 2 lakini kama layman kwani sikufanya utafiti wa kina na nimelimia kilomita kama 300 magharibi ya Dar.
Ninachojua mpaka sasa ni kuwa kwanza ni lazima ujue timing ya high demand,la pili uwe na backup ya irrigation,tatu ni lazima utumie madawa kwa wingi (inashambuliwa mno na wadudu ktk stage tofauti) na la nne ujue kuitumia ardhi vizuri (Nimetengeneza kama majaruba na nikapanda.)
Unatengenenza kama matuta ambayo panakuwa na uwazi katikati na mbegu unapanda katika kingo za hili tuta,yakianza kutambba yanaelekea katika uwazi wa katikati ya tuta.Asante kwa maoni yako mazuri kaka...umeongelea kutumia ardhi vizuri...unavyoongelea majaruba unamaanisha nini?
Na umeongelea pia ishu ya demand...je ni factors zipi zina determine demand? Na high demand hapa dar inakua ni lini...asante