Uncofirmed: Magufuli ameibuka kidedea, kuipeperusha bendera ya CCM

Uncofirmed: Magufuli ameibuka kidedea, kuipeperusha bendera ya CCM

Nadhani watu wanausahaulifu fulani; wamesahau kabisa watu hawa hawa walivyosema Kikwete alipochaguliwa 2005... leo Magufuli kawa jembe?

Hahahaaaa mzee....na bado.

Ataitwa kichwa, mteule au sijui chaguo la Mungu....na kumwagiwa kila aina ya sifa ili mradi tu.....

Mi naona Watanzania wengi ni wepesi mno wa kuvutika na vitu vidogo vidogo mno.

Huyo Magufuli tayari keshawajulia na akianza tu kutema zile takwimu zake watu wanapiga tu makofi bila hata kujua au kuhoji kama ni za kweli au la.
 
Daaah kumbe Magufuli ndo anamrudisha lowasa ICU ujeremani?
 
kama kakatwa lowasa kura yangu ukawa tu cna namna kwa hapa cwezi kumpa mtu kura aliyeandaliwa kuwa mshindi.
 
Dr. John Pombe"Kali" Magufuli vs Dr. Wilbroad Petero "the Rock" Slaa, yeeeees! Tanzania has a chance to reinvent itself with either of the two at the helm, God bless mother Tanzania

mmmh tuseme tu ukweli huyo dokta wako kihiyo angeleta upinzani kama labda hawa jamaa wa ccm wangempitisha mtu kama nyambari chachamaribha nyangwine ndo apeperushe bendera yao ya urais ila kwa hili kamanda lilopitishwa mmmh haina jinsi inabidi tu tuzime fegi zetu mapema
 
aje magufuli aje migiro ukawa ushindi ni lazima sisi hatuangalii mtu tunaangalia na chama alichomo
kina ajenda gani??

ukawa tuna ajenda ambazo hata magufuli hawezi tia mguu hawazi kabisa kufurukuta

1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba

2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu

3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija

5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula

6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation

7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi

8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu

9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe

10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina

11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara

13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi

14 mengine mtaongeze

kwa hayo niliyo yaainisha hapo juu sidhani kama yanaweza kuwemo kwenye ilani ya CCM ambayo kama magufuli ateuliwa kugombea uraisi itabidi ainadi,

kwa mantiki hiyo pamoja na uchapakazi wa maghufuli hizo ajenda hapo juu hawezi zigusa labda kama hajipendi,

kwa jinsi ninavyo wajua ccm kwenye ilani yao watakuja na ahadi za ulaghai, kama kuongeza mishahara, kujenga barabara, kununua meli, na vivuko

ajenda nzito zinzoweza inua uchumi wa nchi kwa miaka mitano hawawezi kuzikubali wakabaki salama
hizo ajenda zitawezekana tu tukiwapa nchi ukawa, kama mnampenda mghufuli mchukueni mkanyywe naye chai
 
Hapo ukawa imekula kwenu!!
Ni Mwananchi yupi asiyejua utendaji wa Magufuli????
Hapo hata muungane na Zitto mumchukue na Lowasa!
Magufuli ni kiboko yenu!
Magufuli ni Mungu mwenyewe kamchagua baba wawatu nazani hata wazo la uraisi hakuwa nalo alikuwa anasindikiza wababe wa hii nchi lakini Mungu alivyomwema hana mfano, Magufuli juuuuu juuu juuu zaidi
 
Hakuna jipya atakalolileta kwasababu hataendesha nchi kwa sera zake, jk walimpa sifa hivihivi lakini tuangalie alichokifanya…
 
Sasa nitatembea kifua mbele
Kazi imeisha kapata zaidi ya 87%! Wale waliokuwa wanasema eti kambi ya EL itapiga kura kwa Amina walikuwa wanaota ndoto za mchana. CCM haiko hivyo, yale majumba ya Dodoma yanakuwa kama yana miujiza manake wanaweza kuingia huko wamenuniana lakini wakatoka wakiwa wanakenua meno kwa furaha wakiwa wamoja.
 
Magufuli ni Mungu mwenyewe kamchagua baba wawatu nazani hata wazo la uraisi hakuwa nalo alikuwa anasindikiza wababe wa hii nchi lakini Mungu alivyomwema hana mfano, Magufuli juuuuu juuu juuu zaidi

n kweli jamaa alikuwa kmya kmya kwenye mchakato wa kusaka wadhamin hakuwa na mbwembwe hata mm nna amin n MUNGU to ndie ameamua awe
 
Kazi imeisha kapata zaidi ya 87%! Wale waliokuwa wanasema eti kambi ya EL itapiga kura kwa Amina walikuwa wanaota ndoto za mchana. CCM haiko hivyo, yale majumba ya Dodoma yanakuwa kama yana miujiza manake wanaweza kuingia huko wamenuniana lakini wakatoka wakiwa wanakenua meno kwa furaha wakiwa wamoja.

Hizo kura unazodai kapata ni kapata kweli au zimepikwa tu?

Maana mkutano wenyewe uliahirishwa ghafla tu kana kwamba tayari walikuwa washapanga kwamba hawatazihesabu hizo kura papo kwa hapo.....
 
Back
Top Bottom