Uncofirmed: Magufuli ameibuka kidedea, kuipeperusha bendera ya CCM

Uncofirmed: Magufuli ameibuka kidedea, kuipeperusha bendera ya CCM

Hizo kura unazodai kapata ni kapata kweli au zimepikwa tu?

Maana mkutano wenyewe uliahirishwa ghafla tu kana kwamba tayari walikuwa washapanga kwamba hawatazihesabu hizo kura papo kwa hapo.....
Mkuu,michakato ya kibongo mingi hasa hii ya ki ccm huwa inaendeshwa kwa imani za kishirikina,ndiyo maana uwazi kwao huwa mwiko.
 
Wajumbe ni zaidi ya 2400,hakuna zilizoharibika??!!

CCM haijawahi kuwa na kura ya haki,ni usanii tu,iwe bungeni,chamani na mitaani,full fitina na figisufigisu za kuhalalisha ushindi

Ni kweli kabisa,na sasa wanaona dhambi ya uchakachuaji inawatafuna wao.
 
Hakuna jipya atakalolileta kwasababu hataendesha nchi kwa sera zake, jk walimpa sifa hivihivi lakini tuangalie alichokifanya…

Watu hawajifunzi na kukumbuka nyuma ilikuwaje. Watu walisema sana juu ya jk,matokeo yake yameonekana
 
mkuu nashukuru kwa matokeo ila hzo kura ukijumlisha znakuja 2611, wakati wajumbe waliopga kura walitangazwa kuwa around 2400, hzo nyingne zmetoka wap? au na wale wachina nao walipiga

si umeshasema AROUND 2400 mkuu au bado tu mnataka pachimbike tena?
 
Magufuli kuingia ikulu ni ndoto za kichaa kujenga ghorofa angani hatowezekana Jk amekubali kuingiza madarakani UKAWA kashfa alizokuwa Magufuli ripoti ya CAG bilioni 262 zimeliwa mtamsafisha na nini?
 
Magufuli akitaka apunguze vikwazo kwenda Ikulu, atangaze atamuweka Mwakyembe kuwa Waziri Mkuu!, hapo atarahisisha njia yake kwenda Magogoni.

Hauwezi muweka Mwakyembe kuwa Waziri Mkuu kwa sababu ya ufanano wao,,wote ni watendaji,,,
Pale anaweza pewa Makongoro kaka,,, subiri utaona
CCM is baaaaack
 
Watu hawajifunzi na kukumbuka nyuma ilikuwaje. Watu walisema sana juu ya jk,matokeo yake yameonekana
Tuiweke pembeni Ccm chama pinzani kichukue nchi ili tuone sera zao kama zinaweza likomboa taifa
 
Hizo kura unazodai kapata ni kapata kweli au zimepikwa tu?

Maana mkutano wenyewe uliahirishwa ghafla tu kana kwamba tayari walikuwa washapanga kwamba hawatazihesabu hizo kura papo kwa hapo.....
Mkuu hakuna kupanga pale hali halisi ilionekana wazi wakati wanaingia na hata wakati wa kujieleza.
 
Back
Top Bottom