Unazikumbuka timu za mtaani enzi hizo?

Miko Villa pande za Mikocheni.

Kwa Sinza,kama baadhi ya wadau walivyosema kulikua na upinzani wa Abajalo (watoto wa Sinza Makaburini,kwa Remmy,Vatican,Palestina) na Sinza Stars(watoto wa Mori,Mapambano hadi Afrikasana). Jamaa walikua wapinzani kweli,pale uwanja wa shule ya msingi Mashujaa ilikua balaa na varangati.

Mpira ukiisha,jioni wachezaji wanakua wakabaji! Duh! Kweli ndondo noma.
 
Duu ....hiyo kali kaka,zamani kulikua na vituko sana kwenye mechi za ndondo,msasani magunia ilikua balaa..

Wewe mtoto wa Kariakoo kule Msasani Magunia ulifata nini?
Yote tisa, kuna jamaa anaitwa Pele, alikuwa anakaa kota za UWT Makumbusho,
jamaa aliwahi kupiga shuti mpaka likachana nyavu pale Magunia..Game ilikuwa East Melin na Sakasaka...
 
Kumbe kaka na wewe wa mitaa hii?
Pale Magunia kuna refa maarufu alikuwa anaitwa Matogwa, jamaa alikuwa anakula hela kwa timu zote mbili, halafu anabalance game inakuwa droo.
Na kabla ya mechi lazima apite kwa washabiki wakorofi huku akiinua tisheti lake ili muone jibisu alilochomeka kiunoni.
Game ikiisha hamgusi mtu hivyo...
 
Faru dume, beach boys, kawe rangers sipati picha enzi za mtoano kinesi cup magomeni, yaani unakuta wachezaji wamekodishwa kuanzia kipa hadi reserve, unakuta kombe la mbuzi but gharama inayotumika kumpata mbuzi ni kubwa mara 20 ya zawadi yenyewe, timu inatumia milion kazaa kwa maandaliz ya kumpata mbuzi au jezi, mitaan raha sana those days

Kwenye kusajila majeshi kuna chama la Mwananyamala linaitwa Daladala Camp...
Hao kikosi chao ni Simba na Yanga tu, labda na wachache wa kataa ambao kweli wana kiwango cha kutisha.
Uliza hala inapatikanaje?
Siku ya game kila daladala pale Mwanayamala kituoni lazima iache buku, na ukigoma lazima wakutie pancha ya makusudi.
 
Hao jamaa noma. Hadi leo bado wapo. Hata Choki muzee ya farasi uwa anawarusha sana kwenye tungo zake.

Ila ubaya wa timu kama hizo ni kwamba zimesheena vikaba. Yaani baada ya mechi kuisha (kigiza kimeshaingia hapo),wanabadili kazi na kuwa wakabaji. Hao Daladala Camp si ndio walioanzisha roba za mbao na ndoo za chuma maeneo ya kuanzia Mango Garden hadi Komakoma.
 
Hapo kwenye red ni kwamba wizi wa aina zote umeanzia Mwananyamala,
kuanzia mchanga wa macho, ndoo, cutting za madirisha, roba la mbao, mtu kati kibabe, n.k n.k
Labda hii mpya ya kuibiwa na kupigwa ngumi nzito wameianzisha watoto wa Keko Gerezani, tena hao wanatumia maguvu na skills zao za kick-boxing, ila wizi wa akili Mwananyamala ndo nyumbani kwake.
 
kweli mwana abajalo nao kitambo mitaa ya sinza wanawakilisha,pia kulikua na sinza star wapinzani wao wa jadi enzi zile,nakumbuka abajalo ilikua na kina kalimangonga Ongala enzi flani hivi.

Jana jumatano ktk uwanja wa Kinesi pale Urafiki klabu hizo mbili hapa nazizungumzia Abajalo ya Sinza na Sinza Stars ya Sinza Madukani zimetoshana nguvu ktk mchezo uliokuwa wa upande mmoja ambao tulishuhudia wachezaji woote wa Sinza stars wakiwa mabeki kwa muda mwingi wa mchezo.

Forza Abuja
 
Miko Villa pande za Mikocheni.

Kwa Sinza,kama baadhi ya wadau walivyosema kulikua na upinzani wa Abajalo (watoto wa Sinza Makaburini,kwa Remmy,Vatican,Palestina) na Sinza Stars(watoto wa Mori,Mapambano hadi Afrikasana). Jamaa walikua wapinzani kweli,pale uwanja wa shule ya msingi Mashujaa ilikua balaa na varangati.

Mpira ukiisha,jioni wachezaji wanakua wakabaji! Duh! Kweli ndondo noma.

NAPINGA HOJA.
Hakuna mchezaji wa Abajalo alowahi kuwa mkabaji.

1. Matokeo
2. Saga
3. Modest
4. George Ngasongwa
5. Baba Dimo.

Huo ni ukuta tu, bado kuna watu walitangulia kama kina Adeba, Abeche na wengine weengi tu.

Pia kuna safu ya kiungo ikiongozwa na Shomali na majemedari wenzie waliokuwa wanakaba, wananyang'anya mipira na kuwalisha watu kama akina Kally, Mfede, Roberto Kalikawe na jeshi Pekee Erick Mzungu ama Erick Cantona aliekuwa anatokea Shekilango FC.

Pia hapo nje kamati ya ulinzi na ushangiliaji iliongozwa na Generali Ayoub Mkobo al-maaruf kama Jean Claude Van Dame.

sasa ntajie mchezaji aliyekuwa mkabaji pale Abajalo.

Forza Abajalo
 
mkuu umekunywa maji ya bendera fo sho!
Umenikumbusha msela wangu Kimwanya, yeye hajui cha Simba, Yanga, sijui Barça wala Manchester,
yeye timu yake moja tu, Texas Dume. Timu ya kitaa chetu Mikocheni Uswahilini.
 
Bila kusahau inter milan ya mtoni kwa aziz ally nyuma ya Sabasaba

Hii timu niliwahi kula nayo tizi nikiwa likizo pale uwanja wa mchanga mtupu-Uwanja wa Sifa (siuji kama bado upo) karibu na kituo cha polisi.
 
Wewe mtoto wa Kariakoo kule Msasani Magunia ulifata nini?
Yote tisa, kuna jamaa anaitwa Pele, alikuwa anakaa kota za UWT Makumbusho,
jamaa aliwahi kupiga shuti mpaka likachana nyavu pale Magunia..Game ilikuwa East Melin na Sakasaka...

naomba nimtetee msasani magunia ulikua uwanja maarufu wa mechi za uswahilini,timu mbalimbali kutoka kila eneo la jiji zilikua zinatimba pale
 
Kumbe kaka na wewe wa mitaa hii?
Pale Magunia kuna refa maarufu alikuwa anaitwa Matogwa, jamaa alikuwa anakula hela kwa timu zote mbili, halafu anabalance game inakuwa droo.
Na kabla ya mechi lazima apite kwa washabiki wakorofi huku akiinua tisheti lake ili muone jibisu alilochomeka kiunoni.
Game ikiisha hamgusi mtu hivyo...

Ilikuwa noma mkuu.
 
Hapo kwenye red ni kwamba wizi wa aina zote umeanzia Mwananyamala,
kuanzia mchanga wa macho, ndoo, cutting za madirisha, roba la mbao, mtu kati kibabe, n.k n.k
Labda hii mpya ya kuibiwa na kupigwa ngumi nzito wameianzisha watoto wa Keko Gerezani, tena hao wanatumia maguvu na skills zao za kick-boxing, ila wizi wa akili Mwananyamala ndo nyumbani kwake.

Mzee hata wakabaji wa Ubungo Darajani wanatumia mtindo huu. Yaani asubuhi unapiga nao tizi (boxing, karate na taekwondo) pale UD-sports ground, jioni wanageuka kuwa wakabaji.
 
NAPINGA HOJA.
Hakuna mchezaji wa Abajalo alowahi kuwa mkabaji.

1. Matokeo
2. Saga
3. Modest
4. George Ngasongwa
5. Baba Dimo.

Huo ni ukuta tu, bado kuna watu walitangulia kama kina Adeba, Abeche na wengine weengi tu.

Pia kuna safu ya kiungo ikiongozwa na Shomali na majemedari wenzie waliokuwa wanakaba, wananyang'anya mipira na kuwalisha watu kama akina Kally, Mfede, Roberto Kalikawe na jeshi Pekee Erick Mzungu ama Erick Cantona aliekuwa anatokea Shekilango FC.

Pia hapo nje kamati ya ulinzi na ushangiliaji iliongozwa na Generali Ayoub Mkobo al-maaruf kama Jean Claude Van Dame.

sasa ntajie mchezaji aliyekuwa mkabaji pale Abajalo.

Forza Abajalo

Kamati ilikua inaundwa na akina nani kama sio baadhi ya wachezaji?
Hiyo kamati na wajumbe wake wakiongozwa na huyo Ayoub Mkobo ndio walikua wakabaji wenyewe mitaa ya kuanzia Makaburini, Palestina na kwa Remmy.
 
Hii timu niliwahi kula nayo tizi nikiwa likizo pale uwanja wa mchanga mtupu-Uwanja wa Sifa (siuji kama bado upo) karibu na kituo cha polisi.
Inaweza ukawa unamkumbuka Dennis Mwang'onda (lotta) alikuwa Inter, pia wapinzani wao Sifa politan
 
Mzee hata wakabaji wa Ubungo Darajani wanatumia mtindo huu. Yaani asubuhi unapiga nao tizi (boxing, karate na taekwondo) pale UD-sports ground, jioni wanageuka kuwa wakabaji.

ni nowmer.
Ila mbinu hizo waasisi wake ni watoto wa Keko Gerezani.
Unajua wale Rashid Matumla amewaathiri sana wale vijana, kila kijana wa Keko anapiga boxing siku hizi...
 
Kamati ilikua inaundwa na akina nani kama sio baadhi ya wachezaji?
Hiyo kamati na wajumbe wake wakiongozwa na huyo Ayoub Mkobo ndio walikua wakabaji wenyewe mitaa ya kuanzia Makaburini, Palestina na kwa Remmy.

Usikurupuke
 
Nshakipiga Panama Fc Mtoni kwa Azizi Ally 1996. Pale nyuma ya uwanja wa Taifa kulikuwa na Likwati FC watoto wa Temeke wailesi nao walikuwa wazuri si haba.
 
Back
Top Bottom