Waandishi Wa Habari Huzitukuza Sana Timu Za Uarabuni..

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,363
9,237
Hello wadau...

Kwa Miaka ya karibuni soka la Tanzania limekua na mvuto mkubwa kiasi kwa sasa ni rahisi tu Kwa shabiki hata wa shule ya msingi kukutajia kikosi cha kwanza cha Simba au Yanga bila kufikiria sana.

Hongera Sana Kwa Azam Media Kwa kuifanya hii ligi kua mubashara hivo imekua rahisi watu kuifatilia na kuiongezea thamani. Miaka ya Zamani watu walikua wanawasikia wachezaji redioni bila hata kujua Sura zao zikoje.. lakini ni tofauti na sasa kwani mchezaji anaweza kua maarufu kabla hata hajacheza Tanzania baada ya kugundulika kua anafatiliwa na klabu moja wapo kubwa. Mfano ni Mkongomani Manzoki alivokua maarufu ghafla baada Simba SC kutaka kumsajili, nadhani pia tekinolojia imebadilisha mambo.

Nirudi kwenye mada. Miaka ya karibuni baada ya uwekezaji, timu mbili za Simba na Yanga zimekua zikiafanya mabalaa kwenye mashindano ya CAF. Ilianza Yanga kipindi cha Manji Kwa kuingia makundi ya kombe la shirikisho 2016 na 2018 lakini waliishia kutoka Kwa aibu Kwa kua wa mwisho kwenye kundi, lakini Kwa wakati huo tayari ilionekana ni mafanikio makubwa.

Baada ya utawala wa Yanga kufa Simba aliibuka Kwa kishindo na kutinga hatua na robo fainali ya CAF champions League ambapo waliishangaza Afrika Kwa kupenya kundi gumu lililokua na Al ahly na As Vita ya DRC bila kuisahau JS Soura ya Tunisia..... Baada ya Hapo Simba amekua hakamatiki kwenye hiyo michuano kila mara japo amekua na bahati Mbaya ya kuishia robo fainali.

Yanga nae ni kama alizinduka usingizi msimu uliopita baada ya miaka minne alirudi tena kombe la shirikisho Kwa kasi ya kimbunga ambapo alitinga hadi Fainali lakini Kwa bahati mbaya alilikosa kombe mbele ya USM Alger ya Algeria.

Katika hayo yote kuna kitu kimekua kikitawala kwenye media zetu pale Simba au Yanga wakitakiwa kucheza na timu toka Uarabuni basi waandishi Wa Habari Huzitukuza Sana Timu toka huko kasikazini. Nakumbuka mechi ya Yanga na Club African mechi ya Kwanza iliisha bila bila, mchambuzi mmoja alisema shughuli Yao (Yanga) ndo imeishia hapo maana anavowajua "Waarabu" Kule Kwao watawapiga Yanga mvua ya magoli lakini mambo yalivokuja kua ni tofauti kabisa.

Simba aliwafunga Wydad Casablanca bao moja bila Kwa mkapa. Waandishi wakaihurumia Simba kua Kule "Uarabuni" kutakua na mvua ya magoli lakini kilichokea mashabiki wa Wydad alianza kulia wenyewe ...

Hivo hivo pia Yanga alipigwa Bao mbili Kwa moja Katika Fainali ya CAF confederation league Kwa mkapa.. waandishi wakasema Yanga amechezea nafasi maana Kule "Uarabuni" Yanga atapigwa nyingi lakini badala yake waarabu walizidiwa Hadi wakaanza fujo ya kupiga mafataki uwanjani na kupoteza muda...

Jana kabla ya game ya Simba na Yanga waandishi walisha ipa Simba mkono wa kwaheri maana walidai Kule "Uarabuni" sio sehemu salama..... Ila baadae mambo yakawa tofauti....

Nadhani sasa ni muda wa waandishi kujitafakari na kuacha kuandika au kuchambua habari Kwa mihemuko. Bali wajikite kwenye uchambuzi na kuziandika vizuri timu zetu sio kuzitisha....

Mambo ya kutishiana watuachie sisi MASHABIKI.... Mimi kama mwana Yanga hata Simba akicheza na timu mbovu toka huko Djibouti lazima ntaitisha Tu Simba japo najua Simba watashinda na mwanasimba pia hawezi kuitakia mema Yanga .. naaam huo ndo ushabiki lakini waandishi nao wamekua kama mashabiki... Inasikitisha sana BADIRIKENI.....

IMG_20231025_093601.jpg
images%20(3).jpg
 
Waarabu wapewe maua yao bhana wako vizuri hawa simba na yanga ni mataputapu tu. Jana nilikua nasikiliza mpira japo sio mfuatiliaji sana ila niliskia mtangazaji akitaja hela wanazokunja wachezaji wa al ahly kuna mmoja anakunja 2 billion sawa na asilimia 10 ya bajeti ya simba kwa mwaka😂😂😂 mwingine anakunja 3 billion kiufupi wenzetu washatuacha mbali na walitutangulia mbali mnooo
 
Hello wadau...

Kwa Miaka ya karibuni soka la Tanzania limekua na mvuto mkubwa kiasi kwa sasa ni rahisi tu Kwa shabiki hata wa shule ya msingi kukutajia kikosi cha kwanza cha Simba au Yanga bila kufikiria sana.

Hongera Sana Kwa Azam Media Kwa kuifanya hii ligi kua mubashara hivo imekua rahisi watu kuifatilia na kuiongezea thamani. Miaka ya Zamani watu walikua wanawasikia wachezaji redioni bila hata kujua Sura zao zikoje.. lakini ni tofauti na sasa kwani mchezaji anaweza kua maarufu kabla hata hajacheza Tanzania baada ya kugundulika kua anafatiliwa na klabu moja wapo kubwa. Mfano ni Mkongomani Manzoki alivokua maarufu ghafla baada Simba SC kutaka kumsajili, nadhani pia tekinolojia imebadilisha mambo.

Nirudi kwenye mada. Miaka ya karibuni baada ya uwekezaji, timu mbili za Simba na Yanga zimekua zikiafanya mabalaa kwenye mashindano ya CAF. Ilianza Yanga kipindi cha Manji Kwa kuingia makundi ya kombe la shirikisho 2016 na 2018 lakini waliishia kutoka Kwa aibu Kwa kua wa mwisho kwenye kundi, lakini Kwa wakati huo tayari ilionekana ni mafanikio makubwa.

Baada ya utawala wa Yanga kufa Simba aliibuka Kwa kishindo na kutinga hatua na robo fainali ya CAF champions League ambapo waliishangaza Afrika Kwa kupenya kundi gumu lililokua na Al ahly na As Vita ya DRC bila kuisahau JS Soura ya Tunisia..... Baada ya Hapo Simba amekua hakamatiki kwenye hiyo michuano kila mara japo amekua na bahati Mbaya ya kuishia robo fainali.

Yanga nae ni kama alizinduka usingizi msimu uliopita baada ya miaka minne alirudi tena kombe la shirikisho Kwa kasi ya kimbunga ambapo alitinga hadi Fainali lakini Kwa bahati mbaya alilikosa kombe mbele ya USM Alger ya Algeria.

Katika hayo yote kuna kitu kimekua kikitawala kwenye media zetu pale Simba au Yanga wakitakiwa kucheza na timu toka Uarabuni basi waandishi Wa Habari Huzitukuza Sana Timu toka huko kasikazini. Nakumbuka mechi ya Yanga na Club African mechi ya Kwanza iliisha bila bila, mchambuzi mmoja alisema shughuli Yao (Yanga) ndo imeishia hapo maana anavowajua "Waarabu" Kule Kwao watawapiga Yanga mvua ya magoli lakini mambo yalivokuja kua ni tofauti kabisa.

Simba aliwafunga Wydad Casablanca bao moja bila Kwa mkapa. Waandishi wakaihurumia Simba kua Kule "Uarabuni" kutakua na mvua ya magoli lakini kilichokea mashabiki wa Wydad alianza kulia wenyewe ...

Hivo hivo pia Yanga alipigwa Bao mbili Kwa moja Katika Fainali ya CAF confederation league Kwa mkapa.. waandishi wakasema Yanga amechezea nafasi maana Kule "Uarabuni" Yanga atapigwa nyingi lakini badala yake waarabu walizidiwa Hadi wakaanza fujo ya kupiga mafataki uwanjani na kupoteza muda...

Jana kabla ya game ya Simba na Yanga waandishi walisha ipa Simba mkono wa kwaheri maana walidai Kule "Uarabuni" sio sehemu salama..... Ila baadae mambo yakawa tofauti....

Nadhani sasa ni muda wa waandishi kujitafakari na kuacha kuandika au kuchambua habari Kwa mihemuko. Bali wajikite kwenye uchambuzi na kuziandika vizuri timu zetu sio kuzitisha....

Mambo ya kutishiana watuachie sisi MASHABIKI.... Mimi kama mwana Yanga hata Simba akicheza na timu mbovu toka huko Djibouti lazima ntaitisha Tu Simba japo najua Simba watashinda na mwanasimba pia hawezi kuitakia mema Yanga .. naaam huo ndo ushabiki lakini waandishi nao wamekua kama mashabiki... Inasikitisha sana BADIRIKENI.....

View attachment 2792069View attachment 2792070
Ni kweli ebu angalia hapa mfano wa Mamelodi na kibonde wake Al Ahyl

Hawa waarabu ukiacha figisu zao,kujiangusha,marefa wa mchongo na mifataki ni weupe kama pamba
20231025_090204.jpg
Screenshot_20231024-195512_Chrome.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom