Unazaa kwa kuwa umejipanga au unazaa tu ili ionekane na wewe una watoto?

Expensive life

JF-Expert Member
May 2, 2020
1,695
5,469
Ndugu zangu Kumekuwa na kundi kubwa sana la vijana kuzaa zaa tu hovyo bila mpangilio wowote.

Nini mantiki ya kuzaa na kuwaleta watoto dunian wateseke? Unakuta mtu anazaa tu kwa kuwa ameona rafiki yake amezaa. Na yeye anaamua kuzaa tu hasa wanawake.

Wapo wanaozaa tu wakishituka kuwa hawakuwa tayari kulea basi mzigo wote huwapelekea wazazi wao huko vijijini na kuwatelekezea huku, kisha wao kubaki mjini wakijivinjari.

Guys kulea siyo lele mama unatakiwa ujipange haswa ili kutengeneza mazingira bora kwa wanao. Kula, kuvaa, afya bora, elimu na mengine mengi. Sasa kuna baadhi wanazaa tu hovyo bila mpangilio wowote kisha kuwapa mateso mazito watoto wao.
 
Umeongea sahihi kabisa wapo wengi wanaozaa ili waonekane wana Watoto, wakishakuwa na Watoto wanaona wamemaliza kila kitu kumbe hao Watoto wanaishi kwa shida.
 
Ndugu zangu Kumekuwa na kundi kubwa sana la vijana kuzaa zaa tu hovyo bila mpangilio wowote.
bila mpangilio wowote kisha kuwapa mateso mazito watoto wao.
Ukiwa na timu kama hii lazima uringe maana hakika umepata Kizazi bora cha kesho kimaisha.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
Screenshot_2024-02-16-11-03-45-93_73617a28b0d3e7e6a04848a88f233e6b.jpg
 
Kama huna hela, upendo mkubwa unaoweza kumuonesha mwanao ni kutomleta duniani.

Watu hawaangalii hata jinsi ilivyokuwa kazi wazazi wao kuwalea wanaenda kichwa kichwa....

Eti 'kukuza ukoo' 'kutekeleza maagizo ya mungu'
 
Kuona tuna mazungumzo kama haya kwenye jamii yetu Kongwe kwenye swala la kupata wowote hata iweje, ni jambo lenye kutia moyo SANA.

Watoto ni Baraka.
Watoto wanakuja na majukumu na utimamu ni kutaka kuweka mazingira mazuri kabla ya watoto kuja.

Ukiona hauna hamasa kupata watoto, sio SHIDA.

(Sina watoto kwa hiari na watu hushangaa kana kwamba nina shida gani sijui .)
 
Back
Top Bottom