Unayotakiwa kuyajua kuhusu battery, chaja za simu na tablet

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,716
39,804
Moja kati ya matatizo ya zama hizi kwa watumiaji wa simu ni uwezo wa simu zao kukaa na chaji. simu zinakaa na chaji kwa muda mchache kiasi kwamba inabidi wajinyime matumizi waache kufanya vitu fulani ili simu iweze kukaa angalau siku moja. ili kupambana na hili tatizo nimeandaa hii makala ili mpaka mtu akimaliza kuisoma awe na uelewa juu ya battery na chaja na wakati mwengine aweze kuchagua simu anayoitaka mwenyewe.

BATTERY YA SIMU
kwa wasiofahamu battery ya simu hiki ndio kifaa kinachotunza nguvu ya umeme inayotumiwa na simu yako na mara nyingi inakaa nyuma ya simu na zipo battery za simu zinazotoka na zisizotoka.
blackberry-bold-9000-battery-1300mah-1.jpg


UJAZO WA BATTERY
hapa ndio pa muhimu sana, battery yako ikiwa na ujazo mkubwa basi kuna uwezekano mkubwa wa simu yako kukaa na chaji sana. ujazo wa battery ya simu unapimwa kwa milli ampere hour au kwa kifupi mah. ina maana simu ikiwa na mah kubwa basi itakaa sana na charge kuliko yenye mah ndogo.

hebu tuangalie mfano hai una gari, gari yako ina tank la mafuta na ujazo wa mafuta kwenye gari unapimwa kwa lita. hivyo unaweza kusema gari langu lina tank kubwa la mafuta hivyo linaweza kwenda safari ndefu bila kujaza mafuta ikiwa full tank.
1. gari = simu
2. tank la mafuta = battery ya simu
3. lita za mafuta = mah
hivyo kwa mfano huo hapo juu tunaona simu inahitaji battery yenye mah nyingi ili kukaa sana na charge.

UIMARA WA BATTERY
uimara wa battery unatokana na cell zilizotumika kutengenezea hio battery. cell imara zinaruhusu kuchajiwa mara nyingi bila kuharibika. kuna battery unaweza kuzichaji hata mara 1000 zisipoteze ubora wake zikawa bado nzima ila battery nyengine ukizichaji mara 50 au 100 tayari zinaharibika. ni vigumu kujua kama battery hii ina cell imara au ambazo sio imara hivyo ni vyema ukitaka battery imara uinunue kwa makampuni yanayojulikana. wale wanaonunua power bank hii pia inawahusu.

OPTIMIZATION YA BATTERY
turudie mfano wetu wa gari tumesema ukiwa na lita nyingi za mafuta basi na gari litaenda umbali mrefu lakini je hili ni kweli 100%?? kuna magari yanakunywa mafuta sana na mengine hayanywi mafuta sana na hili inategemea jinsi kiwanda kilivyo optimize mashine.

kwenye simu mambo yapo hivi hivi kuna simu zina mah kubwa lakini zinakaa na chaji kidogo na simu zina mah ndogo zinakaa na chaji sana na hili linatokana na jinsi watengeneza simu walivyoeka hardware na software zao vizuri. hapa tuchukulie simu nne kama mifano mbili za windows phone na mbili za android, lumia 1520, lumia 1320, galaxy note 3 na xperia t2.

lumia 1520 na lumia 1320 zote mbili zina battery yenye ukubwa wa 3400mah. lumia 1520 ina kioo full hd na processor yenye kasi kuliko lumia 1320 lakini linapokuja suala la kukaa na chaji lumia 1520 inakaa sana na chaji hivyo hapa inaonesha simu zinaweza kuwa na battery sawa ila zikatofautiana muda wa kukaa na chaji
gsmarena_102.jpg

gsmarena_100.jpg

hivyo hapo utaona kuna utofauti mkubwa karibia masaa 32 japo battery zipo sawa.

tukija kwenye android kuna galaxy note 3 na sony xperia t2. galaxy note 3 ina 3200mah wakati xperia t2 ina 3000mah kwa macho ya kawaida utaona note 3 ni bora hebu tuangalie benchmark zinasemaje.
gsmarena_104.jpg

gsmarena_008.jpg

hivyo unaona japo xperia t2 ina battery ndogo ila imeipita note 3.

kwa ushauri zaidi inabidi mtu uangalie simu yenye mah nyingi halafu pia uangalie na review yake ya battery.

EXTENDED BATTERY
tumeiangalia battery vizuri na hadi hapa utakua na idea ya kutosha kuhusu battery kwa nyongeza ni kwamba unaweza kubadili simu yako yenye battery ndogo ikawa kubwa. mfano simu yako inakuja na battery ya 1500mah unaweza ukanunua battery nyengine ya 3000mah ili kuongeza muda wa simu kukaa na chaji.


CHAJA ZA SIMU
umeshawahi kutumia chaja moja ikawa inachaji simu upesi na nyengine ikawa inachaji kidogo dogo? hili tatizo linatokana na kuchajia chaja ambayo ina ampere ndogo. ampere ndio inayokujulisha kiasi gani cha umeme kinaingia kwenye battery na kifupi chake ni herufi A. nitajaribu kuzieka chaja na aina za simu

0.15A-feature phone
0.45A-usb2.0 charging
0.5A-smartphone ndogo
0.9A-usb3.0 charging
1A-smartphone kubwa
2A-tablets

hivyo inabidi kabla hujanunua chaja kwanza angalia battery yako inataka ampere ngapi halafu ununue na chaja ambayo ina ampere kama battery yako. pia unapotumia charger yenye ampere kubwa na voltage zile zile kama battery yako basi simu itajaa chaji mapema zaidi
original
 
Kuna vifaa vingi sana ambavyo vinatumia betri. Kwakuwa betri zimegawanyika kwenye makundi mengi na matumizi mbali mbali, hivyo leo ntaongelea betri za kwenye simu za mkononi hasa hizi smart phone au tablets.

Kwanza kabisa ili betri yako idumu kwa muda mrefu, inakupasa uichaji kwa masaa yasiyopungua 10 mpaka 16 na hata mara ingine inakwambia battery full lakin unakuta sio kweli na muda mfupi baadae inaisha chaji, hapa nazungumzia betri mpya.

Pia usichaji betri iwapo haijapungua chini ya 50% na usiiruhusu betri ikaisha mpaka simu ikazima kabisa, kwa kufanya hivyo mara kwa mara kunaua betri yako.

Na unashauriwa kama unaweza ni vizuri uichaji simu wakati umeizima ili ijae vizuri.

Pia kuna app nyingi unakuta mtu kaziweka ON wakati hazitumii mf DATA, GPS, WIFI au BLUETOOTH n.k hii yote inachangia kutumika kwa chaji ya betri yako.

Kwa wale wenye kusoma emails unashauriwa ui set ichek emails Automatically isiwe kila baada ya dakika 15 au chini ha hapo.

Na kama imehang basi usiizime weka Flight mode OFF then ON kwa muda wa dk 1 au ikilazim basi una ereboot.

Na kama uko eneo ambalo halina mtandao basi pia unasjauriwa kuizima kuliko ikiendelea kukaa on.

Kumbuka kila aina ya betri ina muda wake wa mara ngapi uicharge hivyo basi charging kila wakati unazidi kupunguza kudumu kwake.

Tumia app mf game, camera, music etc pale unapolazimika.

Hakikisha unatumia reccomended charger maana chaji zingine zinachangia kuua betri.

Ili ijae haraka haushauriwi kutumia multiple charger kwa zidi ya simu moja maana kumbuka cable inayoleta huo umeme ni moja ina zile pin ndo zimewekwa nyingi hivyo kunakunyanganyana charge.

Mwingine anaweza kuongezea zaidi.

Jf idumu milele!!!


Welcome to :: KCD Group Limited
 
Mkuu mie swala langu ni hapo kwenye charger ya simu.

1.Umesema ni vema kabla hujaanza kutumia charger, angalua kwanza battery inataka Amperes ngapi ndio ucheki charger yenye output kama hiyo. Sasa, ukiwa unachajia USB uka-connect kwenye port ya computer vipi hapo?

Kwa kuongezea hapo hapo, zile USB cable.zote zinafanana au ziko tofauti? Nauliza hivi kwasababu, mfano una USB cable A, ulinunua na kichwa chake A" sasa nikaitumia hii USB cable A kwenye kichwa cha USB nyingine B", hapo si nisha haribu mambo?

2.Kuna baadhi ya simu nishawahi kuona, ukiwa unachaji ile screen inapungua saa sensivity. Yaani ukitaka kutype huku ipo kwenye charge huwezi, maana screen baadhi ya angle haisupport hadi u-click kwa nguvu saaana, hapa tatizo ni nini? Ata ukionganisha kwenye computer same problem. Hapa shida iko wapi?
 
Unaweza kuiongelea battery ya iphone 5S? naona ina 1500Amh hii si sawa na kuwaibia watumiaji? Kwamba device ni gharama na pia bidhaa ina ubora wa hali ya chini.

Je walitumia vigezo gani kutengeneza simu kama hii pamoja na battery ya aina hii?
 
Mkuu mie swala langu ni hapo kwenye charger ya simu.

1.Umesema ni vema kabla hujaanza kutumia charger, angalua kwanza battery inataka Amperes ngapi ndio ucheki charger yenye output kama hiyo. Sasa, ukiwa unachajia USB uka-connect kwenye port ya computer vipi hapo?
itategemea na simu kama ni smartphone za low end na midrange basi itachaji kawaida tu ila kama ni highend itachukua muda kidogo tofauti na chaja ya kawaida, ila kama una usb3 (port zange zina rangi ya blue) basi itachaji haraka simu yoyote ile

Kwa kuongezea hapo hapo, zile USB cable.zote zinafanana au ziko tofauti? Nauliza hivi kwasababu, mfano una USB cable A, ulinunua na kichwa chake A" sasa nikaitumia hii USB cable A kwenye kichwa cha USB nyingine B", hapo si nisha haribu mambo?
kwa ninavyofahamu ni sawa huharibu mambo ila ni bora zote ziwe ni original tu sababu hizi usb zina standard nafkiri ni umoja wa ulaya ndio ulieka kuwa simu zote zitumie standard moja ndio maana hata simu za nokia zinakuja na usb sawa na samsung hata vichwa vinafanana kasoro logo tu, na wameachana na pin nyembamba

2.Kuna baadhi ya simu nishawahi kuona, ukiwa unachaji ile screen inapungua saa sensivity. Yaani ukitaka kutype huku ipo kwenye charge huwezi, maana screen baadhi ya angle haisupport hadi u-click kwa nguvu saaana, hapa tatizo ni nini? Ata ukionganisha kwenye computer same problem. Hapa shida iko wapi?
sijui kaka tatizo ni nini ila tu nilitengeneza hypothesis kua watakua manufacture wanablock charger ambazo hazijafikia viwango vya battery zao
 
Unaweza kuiongelea battery ya iphone 5S? naona ina 1500Amh hii si sawa na kuwaibia watumiaji? Kwamba device ni gharama na pia bidhaa ina ubora wa hali ya chini.

Je walitumia vigezo gani kutengeneza simu kama hii pamoja na battery ya aina hii?

kaka simu ikiwa ndogo kiumbo (urefu, upana na wembamba) basi hata battery inakua ndogo, kwa ukubwa wa iphone 5s kwenye lumia inalingana na lumia 620
vergelijking-nokia-lumia-620-vs-apple-iphone-5s-16gb.jpg

ila lumia 620 haifikishi hata hio 1500mah hiyo kwa kias fulani wamejitahidi
 
kaka simu ikiwa ndogo kiumbo (urefu, upana na wembamba) basi hata battery inakua ndogo, kwa ukubwa wa iphone 5s kwenye lumia inalingana na lumia 620
vergelijking-nokia-lumia-620-vs-apple-iphone-5s-16gb.jpg

ila lumia 620 haifikishi hata hio 1500mah hiyo kwa kias fulani wamejitahidi

Ninachomaanisha kwanini simu quality kama Iphone 5s ina battery size ya 1500 Amh ambayo ni ndogo sana kwenye kukaa na chaji?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom