Unawezaje zuia usipatikane kwenye simu lakini ujue nani kakutafuta

martyr101

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
363
546
Wakuu si mara kwa mara ungependa kupokea simu ya mtu lakini pia usipopokea na usipokuja kumtafuta baadaye inaweza tengeneza maswali mengi sababu anajua missed call ulipata.

Lakini wakati mwingine inawezekana mazingira ya kupokea hiyo simu siyo mazuri ukaacha ukisema utakuja kumtafuta baadaye ukasahau ni hoja tayari.

Kwahiyo cha msingi ni kutafuta njia ambayo hutapatikana lakini utajua nani kakutafuta na baadaye ukiwa na nafasi nzuri umtafute.
 
*21*0754# kufunga
#002# kufungua apo kila atakaekupgia simu itakua haiingii au kuambiwa namba haipo au namba haipatkan au namba sio sahii lakn msg unatuma
 
Wakuu si mara kwa mara ungependa kupokea simu ya mtu lakin pia usipopokea na usipokuja kumtafuta baadaye inaeza tengeneza maswali mengi sababu anajua missed call ulipata,

lakin wakati mwingine inawezekana mazingira ya kupokea hiyo simu siyo mazur ukaacha ukisema utakuja kumtafuta baadaye ukasahau ni hoja tayar

Kwahiyo cha msingi ni kutafuta njia ambayo hutapatikana lakini utajua Nani kakutafuta na baadaye ukiwa na nafasi nzur umtafute
Simu yangu ukiblock number unaruhusu notification akikutafuta Unajua, kama unatumia Huawei p60 pro sijajua kwa ziingine
 
Hivi kwanini mnakopa halafu kulipa hamtaki jamani? Mpaka unatafuta mbinu humu haya ngoja nikusaidie kuna mwanangu bingwa wa madeni Afrika mashariki na kati kuna namba hizo anatuwekea siku ya mshahara, thubutuuu mtapiga mpaka mchakae ila ye anaona na SMS anapata ila ukimpigoa haiiti wala haisemi haipatikani kimya tu kama bubu ila kule anaona mwenyewe,😅😅😅😅
 
Wakuu si mara kwa mara ungependa kupokea simu ya mtu lakin pia usipopokea na usipokuja kumtafuta baadaye inaeza tengeneza maswali mengi sababu anajua missed call ulipata,

lakin wakati mwingine inawezekana mazingira ya kupokea hiyo simu siyo mazur ukaacha ukisema utakuja kumtafuta baadaye ukasahau ni hoja tayar

Kwahiyo cha msingi ni kutafuta njia ambayo hutapatikana lakini utajua Nani kakutafuta na baadaye ukiwa na nafasi nzur umtafute
Dawa ya Deni ni Kulipa tu Mkuu Oky?
 
Shida mnatenda madhambi sana. Huyo hujamtendea haki. Itakuwa umemkopa hutaki kumrudishia au umtia mtu mimba unataka kuikimbia
 
Dawa ni moja, switch off hiyo laini. Iwe haipatikani, mambo ya hutaki kupokea simu ya mtu na bado utake kujua nani alikutafuta hiyo haina afya.
Kuzima kabisa,Uko ni kuuwa nzi kwa kutumia Bomu you will harm civilians (social media)and infrastructure (important calls and SMS)🤠
 
Back
Top Bottom