MAMESHO
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 1,366
- 1,622
Hapa kutumika namaanisha kuwa kwenye uhusiano kwa sababu fulani ambapo unaona ni kama mtego ambao huwezi kujinasua na unahisi kuna jambo ambalo haliko sawa lakini unaona bora liende na siku zisogee. Hali hii inaweka akili yako kutokuwa sawa na pia unaathirika kisaikolojia. Hizi hapa ni baadhi ya dalili.
1. Furaha yako ya kuwa na mahusiano imegeuka kuwa hofu ya kuachwa. Unakuwa na mawazo na unaonyesha kuchoshwa na uhusiano uliopo.
2. Hali yako inategemea hali ya uhusiano ikoje wakati mwingine unajiskia chini sana na wakati mwingine huna uhakika kama umependa au unajipendekeza.
3. Unajiskia kuharibu kila jambo zuri linalotaka kutokea na hujui kwa nini unajiskia hivyo.
4. Mara nyingi unamuuliza mpenzio kama kila kitu kiko sawa unajiskia kuna kitu hakiko sawa lakini haujui ni kitu gani.
5. Mara nyingi unajilinda sana na unachoongea na unaona kama unachosema unaeleweka vibaya.
6. Umekuwa mpelelezi unakagua simu, unacheki email, akaunti za mitandaoni na kusikiliza kwa makini simu zake.
7. Unajitahidi sana umfurahishe mwenzi wako, unajibidisha sana awe na furaha lakini unaona kama hufanikikiwi hata kwa kiwango kidogo na hujui ufanyeje.
8. Unajiona hutoshi na huwezi kutimiza matazamio ya mwenzi wako.
9. Unajiona huwa unakosea kosea na huwa unaomba samahani mara nyingi.
10. Likitokea tatizo dogo unashikwa sana hasira na unaongea kwa sauti ya juu na hata kulia
11. Unatumia mbinu ambazo huzipendi na ni kinyume na maadili uliyokuzwa nayo ili kumfanya awe na furaha na kushikilia uhusiano.
12.kueleza mawazo yako au hisia kunaonekana kumezuilika na mara nyingi unakaa kimya hata ikiwa kuna jambo hulifurahii au hulipendi.