Unawezaje kujua kama unafanya makosa kwenye matangazo yako ya kulipia? (Facebook na Instagram)

Lazaro Samwel

Member
Apr 27, 2019
33
26
Na wewe huwa unajiuliza swali hili au huwa unaogopa kujiuliza kwasababu unahofia kuona makosa yako?

Ukweli ni kwamba wengi swali hili kulifanyia kazi huwa hatutaki kwasababu tunaona tutajiumiza kwa ukweli ambao tutaujua kupitia matangazo ambayo huwa tunayafanya.

Kuna njia nyingi sana za kujua kama unapoteza fedha zako kwenye matangazo yako ya kulipia lakini kuna dalili moja nyepesi sana ambayo inaweza kukuonesha kwamba unapoteza hela zako tuu kwenye matangazo ya kulipia.

Nisikiliza kwa umakini sasa,kupoteza kwako kwa fedha kwenye matangazo ya kulipia huwa ni matokeo ya makosa flani ambayo huwa unayafanya kwa kujirudia kwenye matangazo yako.

Ndio maana unajikuta kile ambacho unakiwekeza kwenye matangazo yako kinakuwa ni kidogo zaidi ya kile ambacho huwa unakiwekeza.

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema kwamba....

Ukitaka kujua kwamba kuna makosa ambayo unayafanya kwenye ufanyaji wako wa matangazo ya kulipia angalia unachowekeza kwenye matangazo yako na kile unachokipata kupitia matangazo yako.

Kama uliwekeza $25 = 57,975/= kwenye tangazo lako alafu unapokuja kufanya tathmini unajikuta umeingiza $10 = 23,130/= hii ni ishara wazi ya kwamba kuna sehemu unakosea au kuna makosa ambayo huwa unayafanya na haujirekebishi kwenye matangazo yako unayoyafanya.

Na endapo hali hii inajirudia mara kwa mara ina maana unarudia makosa yaleyale kwenye matangazo yako na haujali kujirekebisha.

Acha kwanza nikupe baadhi ya makosa ambayo huwa yanapelekea matangazo yako mengi kukupotezea fedha zao nyingi?

1. Kutokuwa na framework ya matangazo yako.

2. Kutokujua wateja wako vyema na kuishia kufanya matangazo kwa namna yako unayoijua.

3. Kuandika caption ambazo hazina mashiko.

4. Kutumia picha/video ambazo hazina mvuto au hazina mpangilio mzuri wa kile kinachozungumzwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho (Context)

5. Kuweka na BAJETI ndogo kwenye matangazo.

6. Kutokuwa SPECIFIC kwa maeneo ambayo yatakuwa sahihi kwa kile unachokiuza.

n.k

Kuna vitu vingine vya kuzingatia lakini hici naimani vitaanza kukufungua.

Unapenda kushikwa mkono ili usiendelee kufanya makosa haya kwenye matangazo yako na kuendelea kupoteza fedha zako mara kwa mara?
 
Back
Top Bottom