Unawezaje kuishi kwa kipato chako?

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Wakuu salamu.

mimi nimejiuliza maswali haya, nimekosa majibu.

Hivi watanzania tunaishije?

Mshahara wengi wetu 180,000tsh-500,000/ very few in number.
1. mchele 2000/kg
2. unga sembe 800-1000/kg
3. nyama 3000-4000/kg
4. mkate 1000
5. umeme 180-200 per unit( sijui kwa sasa ni sh. ngapi)
6. daladala 600-1200 kwa siku kila siku kwenda job na kurudi home
7. chai+chakula(lunch) 2500-3500 kwa siku ndani ya siku 22 za kufanya kazi kwa mwezi
8. bili ya maji 5000-8000 kwa mwezi.
na mengine mengi.

tuulizane watanzania. tunaweza vipi kufanya hayo yote huku tukimudu kuishi mijini bila shida?

Je hii haiashirii kuwa watanzania wengi hatuishi kwa vipato vyetu, bali tunaishi kwa vipato vya ziada vinavyoambatana na rushwa, wizi, hujuma, utapeli na mengine kama hayo? Hivi unaweza kuishi jiji la dsm kwa mfano kwa laki mbili kwa mwezi?

Nahitimisha na kukaribisha maoni yako kwa kusema, WATANZNIA WENGI NI WEZI, UPENDE USIPENDE WEWE NI MWIZI TU. NI WACHACHE MNO WANAOISHI KWA MJIBU WA ANKARA INAYOPATIKANA KWENYA SALARY SLIP YA KILA MWISHO WA MWEZI
 
Tanzania na watanzania ni zaidi ya uwajuavyo.

Hii ndo bongo bana
 
..na hapo tunalipa kodi ya nyumba 80,000 - 150,000 kwa mwezi, tunasomesha watoto, tunaenda hospitali, tunachangia harusi na kushona sare, tunavaa, tunakunywa bia... kwenye hiyo hiyo laki mbili!
 
Bila kujifunza udokozi popote pale ulipo huwezi kuishi inji hii.
 
Back
Top Bottom