Zionist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2017
- 1,830
- 2,882
Ungefuatilia historia ya hiko kivuko sidhani kama ungeandika jinsi hii, kupinduka kwa kivuko sababu kuu ni kuzidisha mzigo zaidi ya mara tatu..!! sababu ya pili ni watu kukimbilia mbele ili wawe wa kwanza kushuka, hii sababu ya pili ndio ilifanya kivuko kizidiwe uzito kwa mbele hatimae kibinuke. pia lazima ifahamike katika uundwaji wa meli na vivuko huwa wanaunda kwa kubalance chombo endapo kutakua na ongezeko la mzigo na balance ya chombo kwenye u dharura. kwa picha hiyo nafikiri Unaweza kujenga picha jinsi kivuko hicho kilivyokua kimezidiwa na mzigo.Habari kubwa inayotrend ndani ya nchi yetu hivi sasa na nje ya nchi ni kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake huko Ukerewe katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watanzania wasio na hatia zaidi ya 130
Tumemsikia Rais wetu Magufuli kama kawaida yake akiagiza kwa ukali kabisa, hatua Kali zichukuliwe kwa wote waliohusika na uzembe huo hadi kusababisha maafa hayo makubwa kwa nchi yetu
Lakini pia kuna clip moja inayotrend humu mtandaoni kwa hivi sasa ikimuonyesha Mbunge wa Ukerewe kwa tiketi ya Chadema, Joseph Makundi, akilalamika wakati huo Bungeni kuwa kivuko cha MV Nyerere ni kibovu na akaendelea kueleza kuwa aliwasiliana na Waziri wa uchukuzi kwa kipindi kirefu kumweleza tatizo hilo lakini hajasikilizwa, akaendelea kueleza kuwa au ndiyo inasubiriwa kizame kivuko hicho ndiyo waje hapo Bungeni kuchangishana pesa ya rambirambi? Mwisho wa kunukuu
Na kweli hivi sasa utabiri huo umetimia kwa kivuko hicho kuzama na kama alivyoeleza Mheshimiwa Mbunge huyo kuwa sasa ndiyo tuko "busy" kuchangishana pesa ya rambirambi!
Hebu tujiulize kama Taifa ni kweli tunatoa kipaumbele katika vitu vya muhimu kwa Taifa letu?
Au ndiyo tunatoa kipaumbele katika vitu anavyohitaji Mheshimiwa "Mfalme" vipewe kipaumbele?
Hapo ndipo tulipofika kama Taifa, wapo watu watakuwa "victimized" katika tukio hili wakati UKWELI unajulikana kuwa kama Taifa tumeachana na kutoa kipaumbele katika vitu ambavyo kama Taifa tunapaswa kuvipa kipaumbele
RIP wote waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa MV Nyerere huko ziwa Victoria