UNAWEZA KUUA CHAMA CHA UPINZANI LAKINI HUWEZI KUUA UPINZANI

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
611
1,000
Nimesoma kila mahali na kuona kuna watu wanatamani sana upinzani ufe. Hapana hawa watakuwa hawajui dhana ya upinzani.

Upinzani siyo kikundi cha watu ambacho unaweza kukisambalatisha kwa mabomu kikasambaa. Upinzani siyo chama cha siasa ambacho unaweza kukifutia usajili wake au ukawanunua viongozi wake wote halafu chama hicho kikafa. Naam.... upinzani ni nini basi .....nitaeleza

Upinzani ni mawazo ,fikra au mtazamo tofauti juu ya jambo fulani katika jamii. Mungu amewaumba wanadamu na tunu hii ya utofauti wa mawazo. Tangu enzi za manabii wanadamu hawakuwahi kufanana kimawazo hata siku moja.

Upinzani au utofauti wa mawazo upo kila mahali, upo katika familia ,kwenye nyumba za ibada hata maofisini. Utofauti huu wa mawazo ndio umeifanya dunia kuwa hivi ilivyo .Maendeleo ya sayansi na tekinolojia duniani yametokana na utofauti wa mawazo/upinzani.

Kuna watu wanafikiri upinzani ukifa wao wataishi kwa amani na raha mstarehe ,hapana .....nasema tena hapana.

Kuna watu leo ni wamoja kwa sababu kuna upinzani imara .Upinzani ufika hata wao hawatakuwa wamoja tena. Kwa sababu ndani ya kikundi chao lazima yataibuka tena mawazo tofauti/upinzani na kwa kuwa watu hawa hawana utamaduni wa kuvumilia mawazo tofauti ni lazima watagombana na kusambarika vibaya sana. Wataanza kuitana majina ya kila aina.

Upinzani wa kisiasa ni jukwaa la kila raia kutoa mawazo tofauti juu ya jambo fulani. Hili ni jukwaa huru kwa kila mtu mwenye fikra tofauti bila kujali kabila lake, rangi au chama chake cha kisiasa.
Kila mahali kuna upinzani CHADEMA kuna upinzani CCM kuna upinzani ,CUF pia kuna upinzani. Narudia tena kusema mtu hawezi kuua upinzani. Upinzani utakufa siku watu wote wakiondoka hapa duniani.
 
boaz mwalwayo

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
5,770
2,000
Sijui Kwanini CCM wanapenda Sana Kitonga mnooooo! Hawapemdi kujifikirisha

Mkuu si unajua Upinzani una hoji wanataka wauwe Upinzani wawe wanasema Leo tumeokota Ndege aina ya Air Force pale JKN ndio mzee Trump kamipigia cm anataka nimpe msaada wa pesa Marekani imeyumba kiuchumi watu ndiooo sasa Japani wanaitaka niende niwe Rais wao angalau mwaka mmoja nimepewa tahaarifa leo kama za pesa Airport sasa hivi tunahoji ndo tatizo kubwa
 
daudthefarmer

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,494
2,000
Nimesoma kila mahali na kuona kuna watu wanatamani sana upinzani ufe. Hapana hawa watakuwa hawajui dhana ya upinzani.

Upinzani siyo kikundi cha watu ambacho unaweza kukisambalatisha kwa mabomu kikasambaa. Upinzani siyo chama cha siasa ambacho unaweza kukifutia usajili wake au ukawanunua viongozi wake wote halafu chama hicho kikafa. Naam.... upinzani ni nini basi .....nitaeleza

Upinzani ni mawazo ,fikra au mtazamo tofauti juu ya jambo fulani katika jamii. Mungu amewaumba wanadamu na tunu hii ya utofauti wa mawazo. Tangu enzi za manabii wanadamu hawakuwahi kufanana kimawazo hata siku moja.

Upinzani au utofauti wa mawazo upo kila mahali, upo katika familia ,kwenye nyumba za ibada hata maofisini. Utofauti huu wa mawazo ndio umeifanya dunia kuwa hivi ilivyo .Maendeleo ya sayansi na tekinolojia duniani yametokana na utofauti wa mawazo/upinzani.

Kuna watu wanafikiri upinzani ukifa wao wataishi kwa amani na raha mstarehe ,hapana .....nasema tena hapana.

Kuna watu leo ni wamoja kwa sababu kuna upinzani imara .Upinzani ufika hata wao hawatakuwa wamoja tena. Kwa sababu ndani ya kikundi chao lazima yataibuka tena mawazo tofauti/upinzani na kwa kuwa watu hawa hawana utamaduni wa kuvumilia mawazo tofauti ni lazima watagombana na kusambarika vibaya sana. Wataanza kuitana majina ya kila aina.

Upinzani wa kisiasa ni jukwaa la kila raia kutoa mawazo tofauti juu ya jambo fulani. Hili ni jukwaa huru kwa kila mtu mwenye fikra tofauti bila kujali kabila lake, rangi au chama chake cha kisiasa.
Kila mahali kuna upinzani CHADEMA kuna upinzani CCM kuna upinzani ,CUF pia kuna upinzani. Narudia tena kusema mtu hawezi kuua upinzani. Upinzani utakufa siku watu wote wakiondoka hapa duniani.
Mjinga anatumia kodi kununua wajinga wenzie mahitaji ya msingi yanamshinda kufanya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom