Unaweza kupona bila dawa

Mr Lukwaro

JF-Expert Member
Jun 3, 2023
357
621
Magonjwa mengi kama vile mafua na flu, hupona bila dawa.

Njia zenye kusaidia mwili kujikinga na maradhi kwa kutumia kinga yake yenyewe ni zipi?

1. Kujiweka katika hali ya usafi.
2. Kula chakula bora, balanced diet. Kula chakula bora sio ngumu, unaweza pika ugali wako, kula yai moja au samaki kama huwezi kupata nyama mara kwa mara, kula hata tunda moja na kunywa maji safi.
3. Pata muda wa kupumzika.
4. Fanya mazoezi, hata ya kutembea ili misuli iwe active.

Matatizo mengi ya afya husababishwa na mitindo mibaya ya maisha, mfano mzuri ni upungufu wa nguvu za kiume. Hivyo, sio lazima kutumia dawa za kigeni kila unapo umwa au kupata maradhi. Kwa kufuata njia tajwa hapo juu, unaweza kupona, na hata kama utatumia dawa, zitakuwa zinasaidia tu.

Usafi, kula chakula bora, fanya mazoezi, na pata muda wa kupumzika husaidia hata kuongeza uwezo wa kufikiri (IQ).
Screenshot_2023-08-31-22-08-48-97.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom