Unaweza kufaidika zaidi ukiblogu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaweza kufaidika zaidi ukiblogu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Oct 3, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  UNAWEZA KUPATA PESA KWA KUBLOGU

  Nimekutana na rafiki yangu mmoja leo wa siku nyingi kidogo anafanya kazi katika kampuni moja ya huduma za mawasiliano ya simu katika majadiliano yetu tumeongea vitu vingi tu mwishoni akaniambia anapenda sana kublogu lakini hajui ablogu kuhusu nini na muda mwingi anakuwa yuko bored sana hapo hapo akanieleza anapenda kujifunza sana mambo mbalimbali ya ict .

  Watu wengi kama huyu wako wengi sana ambao wanapata matatizo Fulani kwenye kuchagua kitu cha kublogu au kuandika kwenye blogu , huyu rafiki yangu ni mtaalamu kwenye masuala ya Masoko na yuko kwenye kampuni ya mawasiliano ambayo inauza bidhaa nyingi sana za mawasiliano kuanzia simu , vocha na vifaa vingine vya mawasiliano pamoja na kutoa ushauri na yeye moja ya kazi zake ni kuhakikisha bidhaa hizi zinauzika na kukubalika na watu mbali mbali pamoja na hayo kutoa msaada pale anapohitajika kwa bidhaa zinazouzwa na kampuni yake .

  Kwahiyo kama anataka kublogu kitu cha kwanza ambacho anaweza kufanya ni kublogu kuhusu bidhaa za kampuni yake pamoja na huduma mbali mbali zinazotolewa na kampuni yake , mfano tembelea tovuti ya SasaTel hamna sehemu ya blogu pale ambapo kampuni inaweza kublogu au wafanyakazi wa kampuni hiyo hawana blogu zao za kuelezea maisha yao na bidhaa za kampuni yao

  Kwa rafiki yangu huyu yeye alitakiwa kuanza sasa kublogu , kuandika kuhusu bidhaa za kampuni yake kwenye blogu yake kwa sababu atakuwa na uzoefu na bidhaa hizo pamoja na ujuzi wake kwenye masuala ya masoko ataweza kuvuta watu wengi sana watembelee blogu yake pamoja na kuuliza maswali mbali mbali .

  Katika kuelezea bidhaa hizi anaweza kuweka namba zake za simu na maelezo mengine ya jinsi mtu au kampuni Fulani inavyoweza kuwasiliana nae kwa ajili ya kutembeleana au kwenda kuelezwa zaidi kuhusu bidhaa hizo ambazo yeye anazitangaza katika kutembeleana huko kuna ambao watashawishiwa kununua vifaa au bidhaa hizo kwahiyo na yeye atakuwa amepata pesa kidogo kwa ajili ya shuguli hiyo .

  Na blogu ikiwa kubwa sana ikiwa na watu wengi sana kampuni yake hiyo hiyo inaweza kuuziwa nafasi kwa ajili ya kutangaza bidhaa mpya na hata kukusanya maoni ya wateja mbali mbali wa bidhaa hizo hii ni njia moja wapo ambapo mtu anaweza kufaidika kwa kublogu tu .

  Msomaji popote ulipo jua unaweza kutumia ujuzi na utaalamu wako kwa ajili ya kublogu , kuandika kile unachopenda katika blogu yako na kuna wakati unaweza kulipwa na wengine pamoja na kuuza bidhaa zako kwa njia hiyo hiyo .

  Nakutakia usiku mwema leo ukienda kulala fikiria kuhusu kublogu je kama wewe mhasibu unaweza kublogu vitu mbali mbali vya uhasibu na kuuza ? kama wewe ni fundi magari unaweza kuandika kuhusu magari watu wakutafute utengeneze magari yao au kama wewe ni changudoa unaweza kublogu ukapata wateja ?

  USIKU MWEMA
   
Loading...