SoC01 Unavyoweza kufanya biashara bila mtaji

Stories of Change - 2021 Competition

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,440
2,094
biashara.jpg

Picha na mtandao



Usuli
Biashara ni kitendo cha kubadilishana huduma au mali kwa fedha au huduma kwa huduma. Kwa kawaida kumekuwa na dhana kuwa ili mtu aweze kuanzisha biashara yeyote nilazima awe na mtaji au fedha ya kuanzishia biashara hiyo. Jambo hili limekuwa gumu sana kwa watu hasa vijana wanaotaka kujiingiza kwenye biashara hujikuta mawazo yao yakikwaa kisiki kutokana na ukata. Hata hivyo sio sahihi kudhani kuwa kuanzisha biashara kutakuhitaji kuwa na kiasi fulani cha fedha kwani zipo biashara unazoweza kufanya bila kuwa na mtaji au zinazokuhitaji kiasi kidogo sana cha fedha kwaajili ya kuianzisha; Zifuatazo ni baadhi ya biashara hizo;

Biashara ya huduma kwa uhitaji (on demand), Biashara hii haihitaji kiasi cha fedha kuianzisha kwani fedha ya malipo ya bidhaa ndiyo hutumika kuandaa au kuagiza bidhaa. Kwa mfano, unalo wazo la kuanzisha biashara ya mboga mboga, utapaswa kwenda kwa walaji na kuwatangazia biashara hiyo na kuwaomba waweke oda na kufanya malipo, kisha malipo hayo utayatumia kununua mboga kwa wakulima na kuwaletea. Biashara hii inahitaji uaminifu na uvumilivu ili uweze kufanikiwa katika hilo.

Biashara ya uafiliati/ushirika kwa njia ya kidigitali (affiliate program) Biashara hii hulenga kuuza bidhaa au huduma kwa niaba ya kampuni fulani. Biashara hii haikuhitaji kuwa na mtaji ili uweze kuifanya kwani wewe huwa mtangazaji wa huduma au bidhaa na kulipwa mrabaha kulingana na makubaliano. Unachopaswa kufanya ni kujiunga na kampuni husika katika huduma hiyo na kisha utapewa utambulisho fulani na kuanza kutangaza bidhaa au huduma za kampuni hiyo. baadhi ya makampuni yanayotoa huduma hii ni Amazon, alibaba na pia makampuni ya bahati nasibu ambayo hulipa mrabaha kwa afiliati, kuanzia 10% hadi 50% kwa faida uliyoingiza

Kuuza vitabu umeme mtandaoni (E-books) Ikiwa wewe ni mwandishi na huna fedha za kuchapa kitabu chako unaweza kutumia biashara hii kukuingizia kipato. Hariri kitabu chako vizuri na kukiweka katika mpangilio mzuri kisha kipakie katika mitandao mikubwa ya kuuza vitabu mitandaoni. Baadhi ya mitandao unayoweza kuuza vitabu vyako ni, Amazon, lulu, bluu na Google book . Kuuza kitabu chako katika mitandao hii ni bure na hukata mauzo ya kitabu kwa kati ya asilimia 5- 30 kwa kila kitabu kilicho uzika na malipo mengine hurudi kwako muuzaji.

Biashara ya kuuza bidhaa zilizomalizika matumizi, Biashara hii huhusisha uuzaji wa bidhaa au vifaa ambavyo havihitajiki tena kwa namna vilivyo na mtumiaji wake, huweza kuwa ni vyuma chakavu, taka za plastiki nakadhalika. Kuanzisha biashara hii haikuhitaji kuwa na mtaji au huweza kuhitaji kiasi kidogo sana cha fedha kuzinunua na kisha kuziuza kwa bei kubwa. Kwamfano unaweza kununua vyuma chakavu kwa kati ya shilingi 200 hadi 400 na kuziuza kwa kati ya shilingi 1000-1200 na mara nyingine wamiliki wa karakana za ukusanyaji hutoa fedha kwaajili ya shughuli hiyo.

Pamoja na hayo, ili uweze kufanikiwa katika biashara ambazo hazihitaji kuwa na fedha nyingi katika kufanyika kwake nilazima utambue kuwa watu au jamii inayokuzunguka ndiyo mtaji wako. Watu hawa ni pamoja na marafiki zako, wafuasi wako wa mtandaoni, na yeyote anaye kuzunguka.
 
karibu wadau muongeze biashara nyinginezo au swali pia usisahau kuvote
 
jinsi ya kupiga kura kwaajili ya chapisho hili bofya palipoandikwa vote, mwisho wa chapisho
 
Wabongo hawawezi kukupa hela ya mchicha kabla ya kuona mchicha kwenye beseni.
button ya vote haipo nikupigie kura.
 
kama una chochote usiache kushirikisha wadau katika sehemu ya comment
 
kupiga kura kwaajili ya chapisho hili bofya sehemu iliyoandikwa vote mwisho mwa chapisho
 
je ni njia ipi rahisi unayoweza kuifanya kati ya zilizoainishwa hapo?
 
kupiga kura yako kwaajili ya chapisho hili bofya sehemu iliyoandikwa vote
 
Back
Top Bottom