Unaujua Msikiti wa Umawiya? Uliojengwa juu ya msingi wa kanisa?

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,286
1,328
Msikiti wa Umawiya (Kiarabu: جامع بني أمية jami'a bani umaya) ni msikiti mkuu mjini Dameski katika Syria. Ni moja kati ya misikiti ya kale kabisa ilijengwa kati ya 695 hadi 705 BK. Kabla ya ujenzi wa msikiti mahali hapo palikuwa na kanisa la Mt. Yohane Mbatizaji lililobomolewa kwa amri ya Al-Walid aliyekuwa khalifa wa sita katika nasaba ya Waumawiya.

ae562ea047b9fa87f7cf180d77091a0a.jpg



Ndani ya msikiti kuna kaburi la kichwa cha Yohane mbatizaji kilichotunzwa hata baada ya kubomolewa kwa kanisa. Kanisa hli liliwahi kujengwa juu ya hekalu kubwa ya Jupiter na hadi leo sehemu ya kuta za nje ni zilezile za hekalu ile ya kale.

Uwanja ndani ya msikiti umepambwa kwa picha za mosaiki zinazoonyesha miti, majani na majengo kufuatana na mtindo wa Kibizanti na wasanii walikuwa wataalamu Wakristo walioajiriwa kwa kazi hii. Lakini hakuna picha za watu au wanyama kulingana na kanuni za Kiislamu ingawa hata picha jinsi zilivyo hapa hazikuwekwa katika misikiti za baadaye.

09f50ddbdbf88aab9e9566b355a305f9.jpg


Source: Wikipedia or
Great Mosque of Damascus | mosque, Damascus, Syria

~Jodeo~
 
Sio ajabu kujenga msikiti juu ya msingi wa kanisa. Maana uislamu wenyewe ulianzishwa na dola la kirumi kwa kumshirikisha Muhammad.

I'm Just Kidding.
 
Hivi hamuwezagi kujadili masuala yahusuyo dini bila kuweka chuki zenu binafsi,uislamu na ukristo hauhubiri chuki ila waumini ndo mnaharibu.cant yall just get along?
 
Back
Top Bottom