Unatumia sabuni gani kuogea?

Unatumia sabuni gani kuogea?

Nimekumbuka miaka ile, kulikuwa na sabuni nzuri sana za kuogea. Mnaikumbuka Geisha? Sabuni flani hivi kubwa haswa. Ilikuwa sabuni nzuri sana.

Pia kulikuwa Revola, nilikuwa navutiwa na tangazo lake luningani. Pia wangapi wanakumbuka sabuni ya Robert Medicated Soap? Siku hizi hizo sabuni kama zimepotea hivi.

Je, kwa sasa huwa unatumia sabuni gani wakati wa kuoga?mimi siku hizi sijui kwaajili ya ubahili, natumia tu Jamaa zile za Kenya. Wewe je? Tiririka...
Enzi hizo bongo zilikuwa hazipatikani wafanyabiashara wengi walizitoa Malawi.
 
FORTALEZA,
Zamani tulikuwa tunatumia Emperial toka Malawi na Zambia, nyingine ilikuwa kitu kama Vinolia Lavender kama sikosei toka Zambia.Pia Wengi tuliipenda Geisha, na enzi ya shule tulitumiaga Fa Wana wa CHAPUTA wataikumbuka.
Ila sasa hivi nami natumia Jamaa ni sabuni nzuri.
Jamaa si ni sabuni ya kufulia hiyo kwa jina jingine gwanji?
 
Ile jamaa inatosha sana..Nafurahi kuiona famelea yangu one love 🤣🤣
Mimi nilikuwa nakaa kwa uncle ni wealthiest person Ila mambo ambayo sabuni ilikuwa ni jamaa 😁 so nilijifunza kuwa masikini ndo wanahangaika kutakatisha ngozi kwakuwa everything is uncertainty
 
Back
Top Bottom