Unatozwa faini ya Sh. Laki tatu za papo hapo ukikutwa na mzigo bila risiti

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Ndugu wana jamvi ukaguzi wa risiti kwa sasa unafanyika katika mabasi na magari ya mizigo na magari madogo ukikutwa huna risiti unatozwa laki tatu hapo hapo kama hina gari litapelekwa polisi mpaka zitakapopatikana hizo pesa.
Kwa utaratibu huu unatakiwa kila mzigo unaonunua omba risiti vingenevyo faini ya laki 3 itakukabili.

Adumu JPM
 
Kwani wafanyabishara wadogo wenye mauzo chini ya milioni 14 kwa mwaka wana risiti za za EFD? Au hata risiti ya mkono ni sawa? Nkungulume
 
Mbona yule mtoto aliyenunua biskut alikuwa na risiti ya mashine??je angekuwa hana nae angetozwa laki 3 za papo kwa papo?
 
Mbona yule mtoto aliyenunua biskut alikuwa na risiti ya mashine??je angekuwa hana nae angetozwa laki 3 za papo kwa papo?
Hata kwa bidhaa za sokoni kama mchele,karanga, ndizi n.k nazo wanataka risiti?
 
Nchi za Waafrika Wenzetu tu huko Bondeni hata ukinunua Gazeti unapewa Risiti huku kwetu Risit inaonekana kama vile zawadi ya Muuzaji kwa mteja
 
Hapa naona ule urafiki tulioambiwa wa wananchi wa haliyachini ni 0%.kila kuchwao naona yakutubana akina kajamba nani....Haya HAPA KAZA TU
 
Serikali ifanye haraka sana kuwapatia wale dada poa mashine za EFD ili na sisi tunaopata huduma kutoka kwao watupatie risiti kwakuwa huduma zao serikali pia inazijua!
 
Ndugu wana jamvi ukaguzi wa risiti kwa sasa unafanyika katika mabasi na magari ya mizigo na magari madogo ukikutwa huna risiti unatozwa laki tatu hapo hapo kama hina gari litapelekwa polisi mpaka zitakapopatikana hizo pesa.
Kwa utaratibu huu unatakiwa kila mzigo unaonunua omba risiti vingenevyo faini ya laki 3 itakukabili.

Adumu JPM
Kwa sheria ipi?
 
Baadhi ya vitu havina risiti mfn mbao hususani kama unachukua kwa maduka ya vifaa vya UJENZI! Unaweza kujikuta unanunua mzigo hadi m 1 na ushee bila risiti. Unaambiwa nao wanapo zinunua mfn BUGURUNI hawana risiti za efd zenye vat bali risiti za efd zisizo na vat eti kwa sababu wafanya biashara hao hawajasajiliwa ktk vat! Ni ujuha kwa wasimamizi, iweje sehemu nyingine wakusanye kodi hadi kwenye shs 200 za huduma ya choo maeneo mengine washindwe kukusanya kodi kutoka shs 5000 ambayo n bei ya chini ya ubao mmoja? Wanauza mbao ngapi kwa siku? Nani anaye kusanya fedha zaidi kati ya mwenye HUDUMA ya choo na muuza mbao?
 
Wanaouza chini ya Million 14 kwa Mwaka hawahitajiki kuwa na EFD machine. Hao ukinunua bidhaa zao huhitajiki Risiti serikal itoe Mwongozo
 
Back
Top Bottom