Unatakiwa kukomaa na mpango wako

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,227
UNATAKIWA KUKOMAA NA MPANGO WAKO

Ingekuwa kuweka tu mipango ndio kufanikiwa, basi kila mtu angekuwa na mafanikio makubwa sana.

Kila mtu anaweka mipango mizuri sana, yaani sana.Lakini mipango hii haijitekelezi yenyewe, unahitaji kuweka kazi kubwa ili kuweza kuitekeleza.

Kadiri mpango ulivyo mzuri na mkubwa, ndivyo ulivyo mgumu kutekeleza na utakutana na changamoto nyingi.

Na ugumu huu na changamoto ndio zimekuwa zinawafanya wengi kushindwa kuendelea. Kwani wanapokutana navyo huona haiwezekani na kuacha wanachofanya. Kwa kuwa kuweka mipango ni rahisi, basi huwa wanakimbilia kuweka mipango mingine.

Kama utafanya hivi, kila mara kuweka mipango mipya, huwezi kufikia mafanikio makubwa.Mafanikio makubwa utayapata pale utakapokomaa na mpango mmoja mpaka unaukamilisha.

Ukishaamua kwamba hiko ndio unachotaka, basi komaa, hata ukutane na ugumu kiasi gani, usikate tamaa, endelea kufanyia kazi mipango yako.

Kama utakomaa na mipango yako, naweza kukuhakikishia kitu kimoja, ni lazima utaifikia. Kwasababu dunia haiwezi kumzuia mtu aliyejitoa kweli kupata kile anachotaka.

Kumbuka inaruhusiwa kubadili njia, lakini hairuhusiwi kubadili safari, pita popote utakapopita, lakini ufike pale ulipopanga kufika.
 
Mipango inakwenda na nidhamu ya pesa,nidhamu ya kazi na nidhamu ya muda ukifanya hivyo your going to stay in success for a long time.
 
Hakika ni kweli yapasa kukomaa ma mpango kwa muda ili upate kuona mafanikio yake , japo changamoto huwa ni nyingi sana katika kutekeleza mpango uliojiwekea
 
Back
Top Bottom