unataka du dwi tunatoa dwi dwi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
  1. Mashabiki wa Yanga washerekea Krismasi kwa kuifunga 2-1 Simba
    yangasimba.jpg
    Haruna Moshi wa Simba akimzuia Amir Maftaha wa Younga asipate nafasi ya kuupata mpira wakati wa pambano kali lililofanyika Uwanja wa Taifakati michuano ya Tusker.
    broken-heart.jpg
    Sosthenes Nyoni, Vicky Kimaro

    MSHAMBULIAJI Shamte Ally aliyeingia akitokea benchi aliibuka shujaa kwa kufunga bao dakika ya 118 na kuipa Yanga ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Shamte aliyeingia dakika 95 akichukua nafasi ya Abdil Kassimu 'Babi' alipokea pasi nzuri kutoka kwa Ngasa akiwa nje ya eneo la penalti alipiga shuti lilomshinda kipa Juma Kaseja na kutinga wavuni.

    Katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote ulishudia dakika tisini zinamalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 na kulazisha mchezo huo kuongezwa dakika 30.

    Mshambuliaji Jerry Tegete alifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya 60 akipokea pasi ya Abdil Babi na kupitisha mpira juu ya kipa Juma Kaseja.

    Hillay alifunga mabao la kusawazisha kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya beki Bakari Mohamed kumwangusha kwenye eneo la hatari mshambuliaji Emmanuel Okwi dakika ya 79.

    Katika dakika ya 110, Simba ilipata pigo kubwa kwa kutolewa kwa kiungo wake Haruna Moshi Boban aliyepewa kadi nyekundu na mwamuzi Denis Batte kutoka Uganda kwa kitendo cha kutumia maneno machafu kwa mwamuzi msaidizi John Kanyenye.

    Kwa matokeo hayo sasa Yanga itacheza fainali Jumapili dhidi ya Sofapaka, wakati Simba watawania mshindi wa tatu dhidi ya Tusker kesho.

    Mwanzoni wa kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi ya kutafuta mabao ya mapema lakini hali ya kosa kosa iliendelea vile vile hadi pale Tegete alipofunga bao lake la sita kwenye michuano hiyo.

    Yanga iliwatoa kipa Mghana Yaw Berko aliyeumia baada ya kugongana na Mgosi na kumwingiza Obren Cuckovic, pia walimtoa Kigi Makasi kuingia Godfrey Bonny. Huku Simba wakimpumzisha Mgosi na kumwingiza Mike Baraza mchezaji wa zamani wa Yanga.

    Muda mfupi baada ya kuingia Baraza alipiga shuti lilopanguliwa kwa ufundi mkubwa na kipa Cuckovic dakika 77.

    Kiungo Abdil Kassimu alipiga shuti akiwa katikati ya uwanja, lakini hakulenga goli dakika ya 48, naye Mgosi alikosa nafasi ya wazi baada ya kupewa krosi safi na Kanoni, lakini shuti lake likapaa juu akiwa yeye na goli.

    Hadi timu hizo zinahenda mapumziko hakuna aliyebahatika kuziona nyavu za mwenzake, licha ya Yanga kutetawala zaidi katika kipindi hicho.

    Mchezaji wa kimataifa wa Kenya, Jerry Santo alitolewa nje dakika 36 baada ya kugongana na Nadir na nafasi yake kuchululiwa na Ramadhani Chombo 'Redondo'.

    Kinara wa ufungaji katika michuano hii alipoteza nafasi ya kufunga dakika ya 33 aliposhindwa kumalizia pasi aliyopewa na Nurdin Bakari akiwa yeye na goli.

    Simba walirudi mchezoni na kufanya shambulizi la kushitukiza katika dakika 26 pale mabeki wa Yanga walipozani wametegea mtego wa kuotea, lakini Nadir Canavaro alikuwa makini kuokoa hatari hiyo.

    Mwanzoni mwa mchezo huo Yanga walionekana kuwadhibiti vilivyo Simba, lakini washambuliaji Tegete, Kassimu na Makasi walikosa umakini kwenye umaliziaji.

    Mussa Hassan Mgosi akitokea upande wa kulia alipiga shuti katika dakika ya tano lilopanguliwa na kipa wa Yanga, Yaw Berko, dakika moja baadaye Ngasa aliwazidi mbio mabeki wa Simba na kupiga krosi iliyotoka nje.

    Wakizungumzia mchezo huo kocha Kostadic Papic alisema alihitaji ushindi ndicho walichokifanya wachezaji wake.

    Naye Mzambia Partick Phiri alisema soka ni mchezo wa makosa mabeki wake walifanya makosa madogo yaliyoigharimu timu.

    Yanga wailingia uwanjani hapo saa 9:55 Alasiri wakiongozwa na Mrisho Ngasa walienda moja kwa moja hadi golini na kuinama kwa muda kama mtu aliyekuwa akiweka kitu hivyi.

    Simba ilingia uwanjani saa 10:00 Jioni wakiongozwa na kipa wao Juma Kaseja aliyeingia uwanjani hapo na kuwahamasisha mashabiki wao wawashangilie kwa nguvu kabla ya kupiga magoti na kusali.


    MASHABIKI
    Kama kawaida ya mechi ya watani hao wa jadi mashabiki walijitokeza uwanjani kuanzia majira ya saa 6:00 mchana wakijaribu kutaka kuingia uwanjani.

    Nao viongozi wa Simba, akiwemo Katibu mkuu anayemaliza muda wake Mwina Kaduguda na Chano Almasi walionekana wakipita huku na huku kuzunguka uwanja huo kama watu waliopeta kitu.

    Ilipofika saa 7:00 mchana yakiwa bado mageti yamefungwa mashabiki walianza vurugu za kutaka kuingia uwanjani kwa kuvamia mageti lakini askari wa kutuliza ghasia FFU wanawatuliza.

    Kwa kutangaza mageti ya uwanja huo yatafunguliwa saa 8 mchana, lakini bado waliendelea kukaidi na kufanikiwa kuwashawishi walinzi wa uwanja huo kufungua mageti hayo kabla ya wakati.

    Katika harakati za kuingia uwanjani kwa njia za panya mashabiki wawili waliojaribu kuruka ukuta walishia kupokea kipigo cha 'mbwa mwizi' kutoka kwa walinzi walikuwa katika lango kuu.

    Mashabiki wengi waliojitokeza katika mchezo huo ni wale walionunua tiketi za shilingi 5,000 ambazo zilikuwa ni nusu ya tiketi zote zilizotegemewa kuuzwa kwenye mchezo huo.

    Kwa mara ya kwanza tangu Screen kubwa ya uwanjani humu ilipowashwa kwenye mechi kati ya Taifa Stars na Msumbuji.

    Jana mashabiki waliowahi uwanjani humu waliburudishwa kwa kuangalia picha mbalimbali za mbuga za wanyama. Lakini baadaye iligeuka kero kwa mashabiki kufutia kelele nyingi zilizokuwa zikitoa kwenye Luninga hiyo.

    Vitendo vya mashabiki kuvuliwa jezi viliendelea kama kawaida baada ya shabiki moja aliyevalia jezi nyekundu na kuketi sehemu ya Yanga alijikuta akivuliwa nguo yake.

    Kikosi Yanga:Yaw Berko, Shadrack Nsajingwa, Amri Maftah, Bakari Mohamed, Nadir Haroub, Athumani Idd, Nurdin Bakari, Abdi Kassimu, Jerry Tegete, Mrisho Ngasa, Kigi Makasi.
    Simba: Juma Kaseja, Salum KAnoni, Juma Jabu, Joseph Owino, Kelvin Yondani, Jerry Santo, Mohamed Banka, Hilary Echesa, Musa Mgosi, Haruma Moshi, Emmanuel Okwi
 
Back
Top Bottom