Unapohama kutoka taasisi moja ya serikali kwenda nyingine unalipwa fedha?

Wakuu habarini!
Mimi ni mwajiriwa wa wakala mojawapo ya serikali nimepata chance ya kuhamia shirika moja la serikali baada ya kuomba kwa hiari.
Je, kuna stahiki nitarajie kuzipata kwaajili ya uhamisho wangu huu au msemo wa "Hapa kazi tu" ndio niutegemee?.
Hapa kazi tu nimemaanisha hakuna malipo y uhamisho.
Asanteni.
Mkuu habari yako

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu suala la uhamisho japo ni haki ya mtumishi ila maafisa utumishi na wakurugenzi wa taasisi hata wakuu wengine wa idara za serikali wanabana Sana ikiambatana na roho mbaya katika kupitisha barua za watumishi hasa ukiwa unahamia taasisi yenye maslahi zaidi, Kuna figisu nyingi mno kuanzia kwenye hizi taasisi zetu MPAKA utumishi kwenyewe.

Ili mtumishi uhame unatakiwa uwe na barua kutoka taasisi husika unayotaka kuhamia ikionesha Kuna nafasi wazi ya kada yako ( Hapa unaweza kuandika barua kuulizia nafasi katika ofisi unazozipenda, au ulipata fununu kwamba Kuna nafasi ziko wazi hivyo wakishakupa barua ya uthibitisho wa uwepo wa nafasi wazi) unafanya Mambo haya.

1. Unaandika barua ya kuhama ukiambatanisha na barua ya taasisi unayotaka kuhamia ikionesha nafasi uliyopata iliyo wazi ya kada yako, utapeleka barua yako ipitishwe kwa HRO/HOD, CEO au mkurugenzi wa taasisi husika ( hapa huwa Kuna kibembe kwelikweli kupitisha) .Wakishapitisha na kusaini unazituma utumishi ( hapa Kama huna mtu barua yako itaozea kabatini na usipate majibu), lakini ukibahatika kujibiwa na utumishi basi hiyo ndiyo inakuwa ticket yako ya kuondoka. Hii njia ni ngumu mno bila kujuana na watu pale utumishi barua inaweza isijibiwe, ni ngumu kwelikweli na wengi wameshindwa kwa njia hii japo nafasi wazi walipata. Kuna ukiritimba mkubwa pale utumishi.

2. Ukishapata barua ya uthibitisho wa uwepo wa nafasi wazi kwenye taasisi unayotaka kuhamia, unapitisha kwa mwajiri wako then unaipeleka ofisi unayotaka kuhamia Kama utakuwa na uwezo mkubwa wa kuwashawishi na wanamtaka mtu kwa haraka Basi watashughulikia wao ikiwemo kuzituma utumishi, hii njia ni ya uhakika zaidi maana kila taasisi inakuwa na mtu wao pale utumishi kwa ajili ya ku - push mambo yao yaende kwa haraka.., so kwa kupitia wao MDA mfupi barua yako itajibiwa utumishi na itatumwa kwa taasisi yako ili uruhusiwe kuhamia taasisi nyingine.

3.Baada ya taasisi zenyewe kuwa na upungufu wa wafanyakazi kwa wingi, zinatangaza nafasi wazi kwa ajili ya watumishi wa umma kuomba ili wahamie ( hii huwa Kama tangazo la kazi, ila linawahusu watumishi walioko makazini tu), unaandika barua ya kuomba then unaipitisha kwa mwajiri halafu unatuma kwa anuani uliyoelekezwa kwenye tangazo. Wahusika watapitia CV wakivutiwa na wewe wanapeleka maombi utumishi ya kukuhitaji, utumishi wataandika barua ya wewe kuruhusiwa kuhama taasisi, hii ni njia simple Sana haina figisufigisu maana taasisi husika inadeal yenyewe na utumishi.

N:B
Barua ya utumishi huwa haipingwi Wala haina optional inapotumwa kwenye taasisi kuruhusu mtumishi ahame, wakuu wa utawala, wakurugenzi wanakuwa hawana Cha kufanya Wala kukubania zaidi ya kukuachia uende
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri.
Mimi nilienda kumuona mkuu wa taasisi fulani kwa lengo kuhamia pale. Akaniambia andika barua kama kunà nafasi tutakuchukua. Nilipoandika barua kupitisha kwa mwajiri wangu, mwajiri wangu kagoma kusaini hadi niambatanishe tangazo LA kazi au kuhamia.
Hii imekaaje? Nini way forward?
 
Me nadhani dunia ya Sasa haihitaji procedures ili ufanikiwe..
Nadhani tu-push kwa overlap procedures.
Me pia npo kweny harakati za kuhamia sehem ingine...
UTARATIBU NI MGUMU SANA COZ WACHAWI WAPO WENGI WASIO PENDA WEWE UTOKE!
Tuendelee kutafuta tutapata
 
Back
Top Bottom