kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,755
Upo na Computer yako(laptop au desktop).Unaandika mchango wako au mada flani ktk mtandao wa JF.Unaipitia mara mbili mbili au tatu ili kusahihisha makosa ya kiuandishi.Unasahihisha na kujiridhisha kuwa ulicho kiandika kipo sahihi na hakuna kosa lolote.Una-post mada/mchango wako.Baada sekunde kadhaa baada ya kupost unaona makosa ya kiuandishi.Wataalam wa IT tusaidieni hapo,hii kitu inasababishwa na nini?.