Unapata Taswira gani hapa?

RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,751
196
7.jpg



8.jpg


Hapa Kiongozi wa nchi anaonyeshwa wananchi wake wakifanyishwa kazi katika mazingira magumu. Hebu tazama hapo kinamama hao wanabangua korosho bila ya kuwa nyenzo za kazi kwa usalama wao na kiongozi anafurahia tu.

Sasa kama kiongozi alipita na hakuliona hili unategemea hawa wenye kiwanda watabadilika kweli?

Picha kwa hisani ya majengwa blog
 
Hivi si huwa wakienda nje wanaona wanatembelea viwanda vya wenzao? sidhani kama kuna nyenzo duni kama ivi. Hii picha inaonyesha siku iyo mwajiri aliwanunulia hayo magwanda tu akawapa na kiposho flani ili kesho yake waje soap soap kwasababu amir jesjhi mkuu anapita
 
Hatuwezi endelea kamwe! kwa viwanda primitive kama hivyo khaaaaa na Jamaa anaona sawa tuuu
 
Hayo magamba ya KOROSHO naskia ni hatari sana kwenye NGOZ YA BINADAM,YANATOA VIDONDA
 
Hatuwezi endelea kamwe! kwa viwanda primitive kama hivyo khaaaaa na Jamaa anaona sawa tuuu

Wasiwasi wangu ni hao wamama wanaobangua korosho mikono ikiwa wazi , baada ya mwaka mikono itakuwa haitamaniki. Ulizia kitu inaitwa CNSL ( cashewnut Shell Liquid). Ni kemikali hatari sana
 
Ili mradi mkono uingie kinywani baba...sasa wafanyeje...nayeye kwaanza ndo anafikiria safari kwenda Ulaya..... Subiri ikipita siku kumi tangu naandika hii hajasafiri.... niambie .
 
aibu tupu. sina hata la kusema...sijui alienda kufanya nini jamani anawazidishia tu machungu wananchnji...
 
Hivi hizo korosho si zitaunguuza mikono yao jamani? Mashine za kubangua korosho nazo sio kama koti?
 
kilimo kwanza ndo ameanza kuifanyia kazi ameanza na amihogo akafuatia na korosho baada ya hapo ataenda kukagua mashamba ya kitimoto
 
Tena kwa unafiki wa waajiri wa Tanzania unakuta hapo mwajiri amjetahidi kutengeneza mazingira kabla kiongozi huyo hajatia timu. Kweli tutafika? Sasa hapo akiondoka mwajiri hatabadili kitu kabisa manake si hata Rais ameona na hajasema kitu?
 
Hii ni aibu kabisa hi!
Hicho ni kiwanda nacho?
Hawakumpeleka kwa mama lishe mmoja kutembelea hotel yake?
 
Presda anashanga tu na wakati hao wamama wanafanya kazi ktk mazingira ambayo sio salama kabisa!!
Quick look:
1.Hawana gloves-kujikinga na athari za mikono yao from hiyo fluid na michubuko!
2.Hawana safety goggles/miwani-kujikinga macho yao from fluid/maganda-vyaweza kurukia kwenye macho yao na kuleta defets.
3.Etc etc.
OK..Yeye yupo shallow,Je ata hao delegates aliongozana nao hawayajui haya?? Watakuwaje Mawaziri kama hawajui ata just simple basics za industrial safety???...Kiujumla,Hakuna ata just a simple "Housekeeping" ktk kiwanda hicho...wameshindwa ata kumzugisha jamaa!
SHAME!
 
7.jpg



8.jpg


Hapa Kiongozi wa nchi anaonyeshwa wananchi wake wakifanyishwa kazi katika mazingira magumu. Hebu tazama hapo kinamama hao wanabangua korosho bila ya kuwa nyenzo za kazi kwa usalama wao na kiongozi anafurahia tu.

Sasa kama kiongozi alipita na hakuliona hili unategemea hawa wenye kiwanda watabadilika kweli?

Picha kwa hisani ya majengwa blog
Utadhani kiwanda cha chuma chakavu kumbe wanabangua korosho
 
Tatizo hapo ni uelewa wa kiongozi huyu. Sintoshangaa nikisikia kuwa na yeye ana hisa hapo
 
Back
Top Bottom