Wanajamvi habarini za mida? Ninajua tumekuwa tukijadili sana usaliti kwenye ndoa, kizungumputi kilichopo, na mengine mengi. Pamoja na hayo yote, ni kweli kabisa kuwa ndoa nzuri na perfect ziko nyingi zaidi hasa kwa Afrika ukilinganisha ni hizi zilizo kwenye unknown status. Na hata zenye migogoro mingi huwa ni ya mida tu, baadaye mambo yanakuwa murua kabisa! Je wewe unapodumisha ndoa yako kwenye mawasiliano ni mida gani hasa unapenda kumpigia mume au mkeo? unapenda yeye akupigie mida ipi? na unapenda akuambie nini au unamwambia nini?