Unamalizaga usingizi wako wa asubuhi au huwa unaukatisha tu?

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,721
Kuna maisha flani ukiyaishi yaani wewe usingizi kila siku ni kuukatisha tu ikifika mchana ukianza sinzia unabugia tu energy drink kwishaa

Mimi mara ya mwisho kuukatisha usingizi ilikuwa ni kipindi nasoma ila toka niachane na shule kwa asilimia 90 huwa naamka usingizi ukikata ni kuanzia 1:30 asubuhi ndo huwa naamka.

Hii pia ni kulingana na kazi yangu kwani hainilazimu kufungua mapema sana

Humu kuna watu aisee muda wote mchana ukimwambia tu aegemee kwenye sofa mchana hamalizi hata nusu saa anaanza kuota kabisaa.

Sent from my TECNO CA8 using JamiiForums mobile app
 
Kama ni desturi yako kuamka saa 11 hapo huwezi sema unakatisha usingizi maana ni utaratibu ila ungeamka saa nane za usiku ikiwa unalala saa nne hapo lazima ukatishe usingizi.
 
Mfumo wa maisha ya kitumwa ulioundwa na dunia kupitia mfumo wa elimu ndio sababu ya watu kuishi kama machine duniani. Mtu anaamka saa 11 hafanyi ibada mbio mbio anawahi kazini. Akirudi kachoka anapumbazwa na simu na TV kisha analala tena. Ratiba ni ile ile kila siku.

Maisha yanataka uamke, ukae kitandani uyatafakari maisha. Upange mipango, umuombe Mungu. Ukaoge, unywe chai(breakfast).
Saa 1 hivi au 2 unatoka sasa huyo kwenda zako kuitafuta dunia. Tena bora serikalini wana weekend ya Jmosi na Jpili, privates Jmosi unaambiwa half day na unafika nyumbani saa 10 jioni. Hakuna cha off day wala nn wanapumbazwa tu. Kimsingi Jmosi umefanya kazi full time.

Umeshawahi kujiuliza, hivi wewe umeumbwa uje duniani kupiga route ya asbh kazini, jioni bar au straight nyumbani? You are just inclined to an angle ambayo hutoki nje ya cycle hiyo?. Umeshawahi kuamka halafu ukahisi kabisa leo akili, mwili havina ushirikiano kabisa. Si uvivu ni kwamba kweli mwili umechoka, lakini waamka na kwenda tena kazini. Ungekuwa huru hii siku usingefanya kazi, upumzike, afya ya akili ni jambo la msingi sana. Lakini waenda mwisho unakuwa kama mbogo kwa juniors wako, wateja yaani ukali ukali tu.

Sisemi kwamba usifanye kazi, ila binadamu mwenzangu. Jitahidi sana ukifika 45 ufikie stage useme leo siendi kazini na hakuna kitachoharibika, kwa kutoa taarifa au kutotoa taarifa kwa mtu; the latter is much better for your mental health.

Kuna nyakati unahitaji kuwa peke yako tu, just alone. Huu muda unaupata wapi? Jpili hiyo hiyo unatamani upeleke watoto mlimani city.

Ukitaka kuthibitisha watu wanaishi kwa tabu, japo wanajiona wana maisha mazuri. Angalia wakati mtu anapopata sababu ya kutokuwa kazini anavyo enjoy.....anafurahi kweli kweli.
 
Mmmmhh ukweli mtupu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom