Unalikumbuka kundi hili swv

Unalikumbuka kundi hili swv

tamimusalim

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2014
Posts
1,822
Reaction score
499
ImageUploadedByJamiiForums1404574652.887771.jpg ImageUploadedByJamiiForums1404574688.752615.jpg Leo nimewaludisha nyuma katika historia ya muziki uko marekani na kukutana na kundi la s.w.v (sister with voice) kundi hili liliotetemesha kipindi iko lilikuwa likiundwa na wadada watatu,coco, leanne"lelee" na tamala johnson george " taji" ingawa kundi hili halipo tena katika ulimwengu wa muziki duniani hasa muziki wa r&b liliwahi kupata upinzani mkali wakati uwo kutoka katika makundi ya TLC,lililokuwa likitamba na cd yao ya crazy sex cool, pia kundi la X-ESCAPE lililokuwa likitamba na albam yao ya "hook" pia makundi mengine kama jade ,na zhane. Swv katika albam yao walioizindua october 1992 iliojulikana kama "weak" ikiwa na nyimbo moto zilizolipa kundi hilo umaharufu mkubwa kama weak , right here, na kile kibao kilichowaweka katika billboard wiki tano mfululizo kilichojulikana "its about time" ambapo mwanadada coco analalamika kuhusu tabia ya mpenzi wake kuhusu mambo ya kesho kesho!!!
 
Unique sisters ndio walinibamba kipindi hicho!
 
Right here original version ni noumaaa.....SWV walitupagawisha sana enzi hizo......wame inspire mademu wengi sana kufanya muziki wakiwemo watoto wa mzee Ahmed Kipozi "Unique Sisters" ambao ndio kundi la muziki kwa wadada Bongo ambao ubora wao haujawahi kufikiwa na pengine hautakuja kufikiwa baada ya ulimwengu wa muziki kuhama kutoka kwenye makundi........

Hakuna mdada nilikuwa namzimia SWV kama Coco.....Ukimsikiliza kwenye verse ya kwanza ya right here alivyoua lazima umkubali.....
 
Hao si ndio wale walikuwa wanenguaji wa Tancat Almas Okestra katika ule wimbo wa Makumbele au sio.
 
Hao si ndio wale walikuwa wanenguaji wa Tancat Almas Okestra katika ule wimbo wa Makumbele au sio.

Hahaha....unamjua Hilda Waziri weye......unajua nyimbo ya "mawifi"....enzi za vijana Jazz okestra?
 
Da inanikumbusha mbali sana, enzi hizo rock garden morogoro
 
walikuwa na wimbo unaitwa you always on my mind so long time
 
Da inanikumbusha mbali sana, enzi hizo rock garden morogoro
mi nakumbuka enzi hizo radio one ndio ina anza anza wako wapi akina taji liundi na maiko muhagama nisaidieni wako wapi hawa jamaaa enzi zile ndani ya dj show saa nane tulikuwa hatukosi lakini siku hizi amna kitu kila radio ngololo ngololo
 
Hivi hawa swv sasa hivi si ni wazee kweli,Ila muziki wao ulikuwa safi sana
 
Wimbo mwingine wa SWV nilioupenda ni "Lose my cool" waliomshirikisha Redman. In my opinion Coco alikuwa na sauti nzuri kuliko hata Beyonce.
 
coco dont take your luv away ngoma kali sana hii.
swv nakumbuka kitambo kwenye magazeti ya femina toleo la 2000 walitokelezea ukija kibao cha can we na someone ni balaa weka kando right here.
 
kuna kundi la bongo fleva miaka ya 2000 kutoka Mwanza walikuwa wanajiita BWV Boys With Voice nafikiri ilikuwa impact ya SWV katika ulimwengu wa mziki mpaka ikapelekea BWV kuderive jina lao kutoka kwao.
 
Back
Top Bottom