Natafuta matibabu
JF-Expert Member
- Aug 1, 2020
- 262
- 301
Suala la ajira limekuwa ni kilio kwa makundi yote katika jamii hasa wenye vipato vya chini ikiwemo wenye ulemavu wa aina mbalimbali na wasio na ulemavu pindi wanapohitimu elimu zao ama ngazi ya cheti hadi shahada hasa katika utawala huu wa serikali ya awamu ya tano.
Tumesikia kauli mbalimbali hasa za wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza kutusihi tujiajiri bila kuzingatia hizo kauli zinahusu makundi ya aina gani ya jamii(wenye mitaji au wasio na mitaji, wenye ulemavu au wasio na ulemavu).
Kati ya haya makundi, kundi linaloathirika sana ni hili kundi la walemavu wasio na mitaji na serikali ipo kimya bila kuwaajiri.
Nimefikiria sana hii serikali ilipositisha kuajiri wale wanaohitimu masomo yao katika ngazi mbalimbali za kielimu kama ilivyokuwa desturi katika awamu iliyopita, huu uamuzi ulizingatia uwepo wa hili kundi la walemavu kweli? Hivi wanajua hili kundi linavyonyanyasika mtaani? Vyama vya kutetea Walemavu navyo kimya(mara mwisho niliwasikia wanapongeza taratibu za uchaguzi mwaka jana)
Sijajua Sheria inasemaje kuhusu ajira kwa walemavu, hata kama ajira zilisitishwa kwa namna moja ama nyingine ili kupisha mambo mengine kufanyika, hili kundi la walemavu lisingesitishiwa ajira kutokana na uhitaji wake wa kujikwamua katika maisha ya kila siku. Haipendezi mlemavu kajitahidi kapata elimu nzuri ama ngazi ya astashahada stashahada au shahada halafu anarudi mtaani anakuwa mzigo tena ukilinganisha na asiye mlemavu.
Serikali toeni ajira kwa walemavu wenye sifa na uwezo wa kazi kulingana na taaluma zao.