Unakumbuka wapi mdudu huyu?

Unakumbuka wapi mdudu huyu?

huyu tulikuwa tunamwita barareeeee.....huyu bwana tulikuwa tunamtreat kama ng'ombe.....ukiwa nao wengi wewe ndio m'babe.......sasa sisi wakike kukamata wengi tunaanzia wapi.......lazima ukamatiwe.......sasa anayekukamatia inakuwaje.......? ha ha ha......them old days......
watoto wa siku hizi bure kabisa........vitu kama hivi hawana.......

Nakumbuka tukiwa darasa la kwanza na la pili tulikuwa tunawabaka hasa wale wakubwa zaidi kisha tunachimba vishimo vidogo chini tunawaweka na kuwafunika na vioo. Basi wakianza kutembea tembea humo ndani ya vishimo tunafurahi ile mbaya kuwa tunaangalia sinema. Duh! Jamani zamani ilikuwa raha sana! Leo hii mwanangu akiona panzi mkubwa anaweza kupiga mayowe kwa woga!
 
Umenikumbusha. Watoto wamenyang'anywa msamiati. Hata neno uroda lilikuwa linatumiwa sana na watoto lakini sasa hawana uhuru nalo tena. Natamani kuitisha maandamano ya watoto nchi nzima kudai msamiati wao ambao umeporwa na wakubwa. Haki za watoto hapa "zimebakwa".

Ni kweli kabisa watoto wamenyang'anywa msamiati. Tulikuwa tukibembea tunasema 'nasikia uroda' na haikuwa na shida yoyote kusema hivyo.
 
ha ha ha nakumbuka mbali mtoto wa kiume ukiwa uchi utasikia mama anakuambie "shikia nzie yoo"
 
ukikamata wa kijani tunaita umekamata barare mzungu,halafu kuna wale wa nyakati za mvua hawana mbawa wana vistari stari tuliwaita barare komba mavi duh mbali sanaa big up mkuu.
 
Chuo cha Ushirikaaaaa..Moshi those days!!! tulibaka panzi mpaka mwereni kule..old moshi sekondari...daaah..neshno housing...kuzurura tu..!!!

Good Old days...😛layball:
 
nme mwinda sana uyu mdudu...enz hizo nachunga mbuzi
 
............lakini leo hii ngoja umkute akiwa Ofisini kwake anavyojifanya bosi, wakati utotoni kala sana Balanguru.....na kakamata sana balale.
Ahaaaa! Binamu yangu vipi tena mbona unaniaibisha mbele ya vijana?
 
Mkuu we nomaa nimekumbuka enzi hizoooooooooo na marafiki zangu wa kipindi hichoooooooooo na mavazi yangu ya kipindi hichooooooooooo kikwetu tunamwita ''NGALAGA'' na wale wa rangi ya blue ni "KALIMBO".
 
mi nkae kimya, hawa huwaga nawaona kwenye picha, kutokana na maisha niliyo kulia nimemiss vingi.
 
Kizazi cha sasa hakibaki baranguru bali mouse play station .hizi ndizo play station za enzi hizo
 
huyu tulikuwa tunamwita barareeeee.....huyu bwana tulikuwa tunamtreat kama ng'ombe.....ukiwa nao wengi wewe ndio m'babe.......sasa sisi wakike kukamata wengi tunaanzia wapi.......lazima ukamatiwe.......sasa anayekukamatia inakuwaje.......? ha ha ha......them old days......
watoto wa siku hizi bure kabisa........vitu kama hivi hawana.......
Ina maana kila siku wee ulikuwa unabakiwa hayo mabalale/mabalangulu!
 
huku masasi tulikua tunawaita NANTEETE. nakumbuka sana nikiwa chiungutwa miaka ya 1995-1996
 
Back
Top Bottom