Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
hahahaha kweli ni wengi sana tumekimbia tena marathon haswaaaa but akuna aliyewahi kushikwa hata mkono na mkimbizaji lolclass letu lilikuwa halina madirisha ya nyavu wala hakuna frem..ni kama boma, basi ukisikia tu 'manyonya' unachomoka ktk uwazi wa dirisha home hapo hadi kesho....... kimsingi sijawahi kuwaona ila nimekimbia mara nyingi
ushawahi?
Nishawahi nini?
kubanwa na mkojo ulivyokatiza kipori.
Eeeh, ndiyo nshawahi.
We ushawahi?
mi bado.
Lini utabanwa sasa?
unataka nibanwe lini?
Mtondojogoo na nataka ubanwe na mavi na mkojo kwa mpigo ili nikuchezeshe kindumbwendumbwe.
Kindumbwendumbwe chalia
Kikojozi kakojoa na nguo kazinyea
Kikojozi nani huyo
Kikojozi Mwajuma huyo
utantapisha vyuku vyangu ujue. khaaa! halafu inaonesha ulikuwa unajikojolea sana utotoni.
Aaaah wapi. Mi nlikuwa nawakojolea sana akina Mwajuma na akina Hidaya
mmmmmmmmmmmmmh! kwaheri.
Unaenda api?
naondoka zangu we unaongea matusi
Chemwali umenikumbusha mbali.sisi kwetu kuna baba mpaka amekufa tunaamini alikuwa mnyonya damu.
Dah! hii ni moja ya 'hoax' ambazo zilishika hatamu miaka hiyo tukiwa bado makinda...
Nakumbuka nikiwa Mbeya kuna jina la Msekwa(sio Pius Msekwa) lilikuwa maarufu sana...
Na kipindi kile mji haukuwa umejengwa sana kwani kulikuwa bado na ule uoto wa misitu ya mikaratusi...
Sasa ilikuwa inasemekana huyu bwana ni nyonya damu na anatembelea kibito chekundu na hakitoi mlio...
Suala la kwenda shule asubuhi na mapema au kurudi nyumbani kigiza kikiwa kimeingia ilikuwa tafrani sana...