Unakumbuka vioja vipi siku unatahiriwa?


ukaona hapana lazima ujiselfie
 
Atakae anzisha Uzi wa kinyime chake, ndipo nitakuja kukomenti.
Wakubwa watakuwa wamenielewa.
 
mwenye kibamia wa kwanza kuwa proudly hadharani, hongera kaka angu
Basi itakua tunapishana majukwaa. Ila humu nilianzisha hadi movement niliita #IamTiny tukafanya kikao na kuna uzi wetu kabisa. Nikachaguliwa kua mwakilishi kanda ya Pwani wa Chama cha SDU (Short Dicks United) chenye makao yake Nairobi.

So I have always been open about this.

Am so sorry haukuwahi kujua kabla ya leo.
 
Sijui hata ilikuwaje,mi nilikuwa najuwa ndio nimezaliwa hivyo hivyo,baadaye ndio nikaja kujua kumbe waliniwahi kabla sijawa na akili timamu...
Sitakuja kuisahau hiyo siku kwa kweli. Walaaniwe wale jamaa.
Dah! Nilikuwa darasa la tatu!
Tulikuwa kama watoto 6 mtaani kwetu.

Mwanaume anatakiwa atahiriwe kwa kisu, hadharani, umetulia bila kutikisika wala Kutoa chozi hata kidogo. Sio hizi hadithi za ngazi na sijui madakitari.

Mwanaume usipotahiriwa hivi, unakuwa umezidiwa na binti aliyekeketwa.

Inaonyesha kusingekuwa na hospital wengi wenu mngekuwa na mkono wa sweta.
Your browser is not able to display this video.
 
Jamaa walinisimamisha kwenye sehemu iliyo na siafu pasipo mimi kujua. Ile kufika usiku kumbe bwana siafu kaingia mtaa wa Magogoni. Kile kilio ilibidi asubuhi nikasalimishwe hospitali, njia ya kumtoa huyo bwana siafu ilibidi nitahiriwe tu. Na mlaaniwe nyie jamaa mlionisimamisua kwenye siafu popote mlipo.
 
nilipelekwa na mamdogo kununua gari la tipper kufika hospital akantoroka nkakutana na mdada nesi mzurii...Akaniingiza wodini basi akiwepo yeye silii akitoka nalia dah wakanikata dushe nikawa natembea na kanzu tu
 
Nyakati zinabadilika ndugu hapo kabla kulikuwa na simu za mezani baada Miche,sahivi touch.. usikariri binadamu anaenda kwa ufahamu kuna muda ila ilimradi tu tusiiharibu nature laws,Kuna watu wametahiriwa hospital na wanaujasili kushinda huyo uliomuweka hapa jifunze kitu kinaitwa saikolojia ya binadamu utanielewa namaanisha Nini.
 
kivipi mkuu? Yaani mimi niliyesimama naangalia mbele huku ngariba anafanya yake bila hata kutikisika nijidhalilishe kwa huyu aliyepigwa nusu kaputi ndo akakatwa?
ni kujidharirisha Sana, mtu uliyesimama tuli huku ngariba akifanya yake kuchangamana na watu waliochomwa ngazi halafu anajisifia kuwa kaenda jando.
 
kupigwa ganzi ni umama, mtu aliyepigwa ganzi status yake ni sawa na binti aliyevunja ungo, binti akivunja ungo anajikuta tu damu inatoka bila maumivu yoyote.
Faida za kutahiriwa bila ganzi ni nini...?
 
Aisee baada ya siku kadhaa baada ya kukatwa govi, yaani ile alfajiri nikidindisha dudu linauma balaa, sitasahau
 
Mimi nilikuwa darasa la nne.. Nilifungwa macho nikapigigwa ganzi... Nilikuwa nasikia sauti za mikasi tuu... Baadae nafunguliwa naona imevalishwa plasta


Kile kipindi nilikula bata sana, kila mtu alikuwa ananijali
 
Mimi nakumbuka baada ya kutoka hospital nilikua na babu yangu, yeye akafuata mishe zake mimi nikarudi nyumbani. Sasa kabla sijafika hom acha nikutane na mbwa wengi. Ikabidi nisimame kwanza hapo mikono ipo mfukoni naugulia maumivu. Mbele hamna mtu, nyuma hamna mtu kukimbia siwezi. Hapo mbwa wananibwekea huku wananifuata. Nikasema hapa kilichopo akinisogelea nampa buti moja sitajali kama nitaumia. Bahati nzuri haooo wakasepa migombani huko. Nikavuta pumzi nikaendelea na safari. Mshumaa wa Mbao,
 
kweli kabisa wakati umebadirika, ndio maana wanaume wanaolewa siku hizi Kwa kisingizio cha usasa.

 
wale wa kimila kuna msoto usio na maana. Picha linaanza siku mnatahiriwa mnajengewa kabisa geto la mabua na choo chake mbali na nyumba ili msichangamane. Baada ya ile shughuli kufanyika mnafungwa vitenge kiunoni kifua kikiwa wazi, unapita wembe kichwani bonge la upara halafu mnapakwa matope kuanzia kichwani mpk kiunoni na miguuni. Mtu akishapakwa hilo tope ndo hakuna kuoga mpk mwezi uishe ambapo kuoga ni siku ya kumaliza jando. Maisha ya jando sasa kinachoendelea uko ni mnapoamka asubuhi inatakiwa muondoke mkashinde porini kurudi muda wa msosi mchana, huko porini ndo kufundishana maadili wenyewe wanavyosema japo imetawala misemo fln ya kiluga ambayo ni fulu matusi wenyewe wanaita mizimu, ukiulizwa muzimu na huna jibu basi ni stiki zinatembea haijalishi umefundishwa ama laa, baada ya stiki kama huufahamu huo mzimu ndo utapewa jibu. Stiki zenyewe zinachongwa halafu zinawekwa kwenye moto zikiwa za moto ndo mnaulizana ukikosa inatolewa kwenye moto/majivu unachapwa nayo kwa kufuata mishipa ya mikono yaani inapigwa parallel to veins. Kuna mambo mambo mengi sana ya kiboya huwa yanaendelea huko lakini yote lazima utii iwe umeonewa au laa. Tena ile siku ya kwanza mnatahiriwa tayari mnapewa majina/vyeo kulingana na umri pia mnapewa na kiongozi wenu wa kuwapeleka porini, kuwafundisha na kuwafuatia chakula kwamaana kipindi chote hicho haitakiwi kuonana na wanawake, mkipita mtaani basi macho chini kwa mstari huku mkiimbishwa mapambio ya kilugha. Ikitokea mpo porini mmekutana na mwanamke asiyeolewa bado basi inatakiwa awaheshimu kwa kukimbia asipofanya hivyo mnaruhusiwa kumpiga. Ubaya wazee washapitisha hayo yote so hakuna anayepinga wala kubisha yaani kifupi ni kama all kinds of umama hakuna kabisa hata uonewe na kiongozi bado hauna pa kulalamika. Kuna wadau wanatokaga huko wakiwa wamepata alama za viboko mikono yote kama tatoo kumbuka unachapwa kiboko kikiwa cha moto. Kuna ishu ya msosi pia kula ni lazima hakuna kusema nimeshiba mpk kiongozi aridhike tena kuna ujinga mwingine ile msosi unaletwa ugali ukiwa kama mlima hlf kiongozi anachoma katikati mnatakiwa kula mpk lile tundu lifutike na akijisijia kuongeza anaongeza wala hakuna wa kumuuliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…