YAH:KUKANUSHA TAARIFA ZA UONGO DHIDI YA MWL KINSHULI:
Hbr ya Leo wanabodi!
Tangu Jana jmosi tar.11/11/2017.majira ya SAA kumi jioni viongozi wa mwanza sec,Kuanzia Mkuu wa shule,Wasaidizi wake na walimu kwa ujumla tumepokea simu nyingi sana zikitaka kufahamu ukweli kuhusu kugongwa Gari Mwl wetu Kinshuli na kufariki dunia.
Ukweli ni kwamba Kinshuli yuko salama salimini kabisa.Anaendelea na harakati zake za maisha. Aidha kwa Bahati nzuri Jana Mwl Kinshuli hakufanya mazoezi yake wala kusafiri kwenda mahala popote.Hata hivyo mbali na kusikitika kwa taarifa hizo za Uongo tunafuatilia kujua chanzo cha Uvumi huuu.
Kwa kupitia jukwa hili naomba litumike kusambaza ujumbe huu wa kukanusha Taarifa hizi za Uongo,Dhidi ya Jemedali wetu wa michezo ya Riadha na mtaalamu wa kufundisha somo la Historia.Mwl.Jeremiah Kinshuli.
Wasalaam!!!
Abel Dendwa.