Ufagio unanikumbusha shule ya msingi kufagia eneo lako. Nilipata bahati mwanafunzi mmoja maeneo yetu yalikuwa jiran jirani akaniambia mie nitakuwa nakufagilia na kwako huna sababu ya kuja mapema nikabaki na tabasamu tu. Wiki ya kwanza nikawa na wasiwasi anaweza asifagie eneo langu nikawa bado nafika muda ule ule. Akaniuliza mbona bado unawahi si nimekwambia nitakuwa nakufagilia kila siku. Nikaongeza 1 hour ya kufika shuleni. Baadaye tulipoingia madarasa ya juu maeneo yetu yakawa mbali mbali. Akaniambia kule kwako mbali siwezi tena kuja kukufagilia. Ikabidi nianze kuwahi tena
Hahahahah si useme tu alikua mchuchu wako! Yaani akufagilie tu bure bure kuna mushkel kidogo lol