Unakumbuka nini ukiona hii

Me nakumbuka kipindi cha mama na mwana kilikuwa mchana mara nyingi wakati huo nilikuwa nawait chakula, na mother yuko jikon anapika.

Kipindi cha Klabu Raha Leo siku za Jumamosi, jioni Wakati huo radio ni RTD pekee na idhaa zake.
 
Hiyo ndo ngoma bwana nilikuwa nikigusa tu nalambwa 5 eti ntaharibu redio do sasa cd mabroo na wajomba bwana
 
Nakumbuka radio hiyo ilikuwa getho ya braza mmoja ambaye alikuwa anatupa ufunguo na ss tunaenda kuwaadhibu wanafunzi wenzetu tukiwa sekondari.
 
Wimbo huo wa Ntombi ulinifanya niwe mlevi kupita kiasi, ukitoka huo anakuja Mzee wa ende inde, inde moniii-Kanda Bongoman, halafu Arlus Mabele; ila sasa nakunywa kidogo tu

Hahahahahhh inde by kandabongomani nilikuwa naucheza wote kama wanavyocheza wenyewe
 
Pia nimekumbuka nyimbo ya M mshehe wa jogoo la shamba aliwik mjini.nilikuwa na jamaa mtaani kwetu anajifanya mbabe sana na kupiga watu ndio akiimbia hiyo nyimbo mapaka mwisho akapewa jina la jogoo wa shamba.
 

enzi hizo kulikua na vitu vya kina Nguashi Ntimbo na orchestra vestival du zaire: Shauri yako.

Shauri Yako by Nguashi Ntimbo, orch Festival du Zaire / original - YouTube

Sam mangwana: maria tebo:

Sam Mangwana_ Maria Tebbo - YouTube

Tabu Ley: Maze:

Rochereau Tabu ley - Maze. - YouTube
 
Nakumbuka redio hii niliinunua kwa mara ya kwanza mwaka 1992,mwaka 2001 iliunguzwa kwa radi lakini nikanunua nyingine kama hii mwaka huohuo na bado ninayo.
 
Nadina yoo nadina mama, rudisha mwili na roho nyuma mamaaa
Mimi pasi nipooo, roho inadundaaa,
Heee yoo nadiina yeyeee, unipe mapenzi yako yoteee eee

Ngoma imenoga hapo ghafla unaskia kwichikichikwichiiii, ukifungua kanda ishasokotwa kitamboo. Inabidi uitoe pole pole utafute ki screw driver kiduchuu uifungue, urudishie na wakati mwingine kama imetafunwa sana unakata kile kipande na kukitoa kabisa, unafunga na kurudisha utumbo ndani kwa kutumia pen ya BIC, unaendelea kula ngoma....
 
Mi inanikumbusha like kipindi cha

Keyiii keyii shangaziiii.
 
Dah, sad memory. Nikiwa std 1 niliugua malaria muda mrefu. Nikawa napewa klorokwini. Aisee, kutwa nzima najilaza nasikiliza redio. Saa ya malenga watu nadhani ilikuwa saa ya dawa. Basi wakiimba mashairi kile kisauti chao naona kama wanashare huzuni zangu. Jumapili ilikuwa kipindi cha wagonjwa, lol. Last year nilijikuta kijijini na safari ya muda mrefu, na the only station ilipatikana ya tbccm na kipindi cha wagonjwa. It was a walk on the memory lane!
 

Baada ya kipindi cha majira, kinafuata chubuku hongera hongera hongera, then inakuja mzee jangala, na kina mzee mundu.
By the way unakumbuka jumapili mchana KBC, kipindi cha jee huu ni uungwana, cha leonard mambombotela?
 
Me nakumbuka kipindi cha mama na mwana kilikuwa mchana mara nyingi wakati huo nilikuwa nawait chakula, na mother yuko jikon anapika.

Asikwambie mtu kitu cha ARTECH, kule kwetu wakati tunatafuta maisha tulikuwa tunasafiri toka Mbeya kwenda kufanya vibarua vya kukata miwa kilombero, mwisho wa msimu unarudi na Hiyo makitu au baiskeli za Shang zheng, ukifika home lazima mchumba ajilete kuolewa, dah! those old good days, Unatumia battery ya gari as source of power
 
Kipindi baba kanunua ya aina hiyo, kanda ya kwanza kununuliwa na kaka yangu mkubwa ilikuwa na nyimbo za 1. kajituliza kasuku 2. Dunia duara 3. Sisiri na nyinginezo. Umenikumbusha mbali sana mkuu na redio ilikuwa inawashwa baba akiwapo tu, akienda kazini anategesha namba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…