Unakumbuka nini enzi zako za Chuo kikuu?

Nilienda kupiga pepa la UE Coet. Kufika mlangoni Naulizwa ID kujisachi hamna. Bila ID huingii. Nikawaza akili ikanituma nikaenda hospitali ya chuo. Nikaongea na dereva wa ambulance nikampa 30,000/=. Akanifikisha Mabibo chap na kurudisha main campus.
Itaendelea...
Ilikuwa hamna boda boda
 
Sikumbuki kitu zaidi ya kuishiwa hela ndani ya week toka zitoke hapo kwa waliosoma under MOF wanakumbuka kuwa hela ilikuwa inatoka ya mwaka mzima.

Msoto wake sina hamu nao.
 
Nakumbuka Mwaka wa mwisho maisha yalikuwa magumu sana hivo Msimu wa Mihogo tulikuwa tunapeana zamu na wana kubeba Mihogo maana tulikuwa tunakaa Hostel za nje kwenye begi kuja nayo chuo tukifika tunajichimbia vimbweta vya mbali tunapiga Mihogo yetu ya Kuanza Pindi na inakuwa tushaua winga Mpaka usiku hiyo sasa kuna mademu walikuwa hawatuelewi tukashangaa baada ya week na wao wanasema Kesho njoo nayo Mingi na ndipo urafiki ulipoanza.Dah Maisha haya
.
Umenikumbusha udsm wakati uko choka mbaya unafanya miamala ilikuwa noma kweli kupita na kimfuko umebeba wali+ mchuzi unajifanya mgumu kumbe umepigika kichizi
 
Nachokumbuka ni kwamba sikuwahi kuijua maktaba chuo mpk naenda kusign zile clearance ndo nikaelekezwa kila mtu alikua haamini napo muuliza..

Nakumbuka pia tuliwahi kuforge cheti cha kifo ..sababu tulishindwa kufanya mtihani maana Jana yake tulikua club usiku kucha..halaf pepa yenyewe ilikua ya Econometrics
 
Nilikuwa ni miongoni mwa 'john visomi' wazuri tu darasani na nilikuwa ni kiungo mchezeshaji mzuri sana wakati wa mitihani. Sitasahau kuna paper moja ilikuwa ngumu sana isitoshe invigilator alikuwa mnoko na alikaza kwenye kusimamia, 'wadau' wengi waliotegemea 'kupiga chabo' walitoka hola siku hiyo.
Baada ya pepa nikawapa moyo paper ya leo 'tight' hata mimi 'sichomoi' kivumbi matokea nna A matata wakati 'wadau wangu' hali mbaya. Long Live SUA.
 
Nilikua na jamaa angu pale Udsm tukisoma wote education. Jamaa alikua anapenda sana mademu, sasa alikua hapendi kabisa wale mademu zake wajue kuwa anasoma education. Toka tunaanza chuo mpaka tunamaliza alinipiga mkwara kutoongelea mambo yanayohusu education pindi akiwa na mademu zake.
hahahahah umenikumbusha jamaa yangy wa BELM (Education ) iko mzumbe, naye alimpenda mtoto wa HRM hapo kuna hesabu (qms 100). jamaa kila siku namshangaa anahangaika ku solve paper wakati wao hawana hesabu.

kuja kugundua alimdanganya demu anasoma BAF hivyo hesabu haimpigi chenga. demu kugundua akambwaga. hawa watu wapo mkuu
 
Yani katika sred nilizosoma kuanzia page ya kwanza hadi ya mwisho ni hii. Binafsi sitasahau ishu mbili zilizonitokea chuoni, moja ni pale tulipokuwa tumefulia me na jamaa yangu, so ikabidi tuwe tunanunua msosi wa buku tunapiga featuring, sa kumbe tukawa hatushibi bwana, siku moja nimeenda kugegedana na demu wangu ambae ndo wife kwa sasa, mara paaap!!! Mashine ikagoma kuamka. Ikabidi show iahirishwe, kwenda kwa Dr akaniuliza km nakula nashiba, nikamwambia huwa nakunywa chai, mchana deshi af usiku tunakula msosi wa buku watu wawili. Akanambia make sure unakula 3 times then jipange mkapige tena show, weeeeh kilichoendelea wife hakisahau hadi leo. Maisha ya chuo buanaaa!!!!
 
Mi nakumbuka semester ya kwanza supp
Ya pili supp
Ya tatu sup

Ya nne wakaona namaliza makaratasi nikadisco.

2020 Mungu akipenda naanza Open japo nimezeeka ila degree naitamani.
Haaa haaa...pole mkuu, first year ukianzaga na masupp, kudisco inakuwa rahisi sana sijui kwanini!
 
Maisha ya Saut yalikuwa matamu sana, nikikumbuka mashindano ya Fawasco, Prolife, nikikumbuka kusumbuana na washikaj kwenye kuandaa assaignment kwenda kupresent, quiz za kushtukiza, kuwa na kipindi siku ya Jmosi tena saa 9 mchana.

Sitasahau kamati kwa wale waliosoma Saut wanajua "kamati" "mzora" wakati wa UE bila kusahau kula raha ndani ya rock city hapo club lips, charcoal libs,stone, Shafik beach, nyumbani hotel, Rock&roll, villa park, The kiss, Rock Bottom etc

Tukio nisilolisahau dah tulipigwa supp ya course inaitwa photojournalism chini ya lecturer Rubaba alitufanya mbaya karibia nusu ya darasa walirudia hapo ndio unajua uchungu wa September conference
 
b2ap3_large_college-student---36234671.jpg


Mimi nakumbuka nilikuwa mtaalamu sana wa viapo ambavyo hatitekelezeki enzi hizo.Nilikuwa na mipango mingi sana napofika chuo nasema semester hii nitasoma sana kuliko kawaida ila mwisho wa siku maisha ni yale yale ya kuanza kusomea mtihani tu aka ZIMA MOTO hahahaha ilikuwa noma sana hasa pale mtihani wa UE ukikaribia.

Siku nayoamua kusoma nanunua kabisa na Backup(Mkate wa kula usiku wakati nakesha napiga msuli) ila mda unapofika nafungua slides halafu nafungua na mkate then nakula mkate nashiba kabisa then napanda kitandani nalala nikiwa nimeshiba tena bila kusoma(Hahahahaha).

Inapofika kesho yake nakumbuka kuwa jana sikusoma naanza kujutia na kuapa kuwa LEO lazima kieleweke mara paap sms ya mrembo inaingia tunaanza kuchati na ndio mambo yanakolea tunaelekea kutoboa...Mara siku imeisha na mtihani kesho!



Wakuu hebu tujikumbushe kidogo ilikuaje kuaje enzi hizo ukipambanana na maisha ya chuo?
Daaaaah apo kwenye mkate umenena mkuu
 
Nimeingia kwenye paper kichwa " empty" jirani yangu nimekaa na mtu wa makamo anaonekana john kisomo kweli.Navuta muda kwa kugeuzageuza karatasi ya maswali huku nikiwaza namuingiaje anipe majibu.Na yeye yupo kimya anapitia karatasi ya maswali kwa utulivu mkubwa,najipa matumaini huyu ndio mkombozi wangu lazima nipate hata C.Muda unakwenda kasi sana mara nusu saa inakatika sio mimi wala yule mzee anaandika,mara saa moja linakatika hali ni ileile.
Naanza kuona hali ya baba wa Taifa inakuwa mbaya ,najilipua maswali yote chuma.Najibu swali la kwanza ,naanza kujibu swali la pili mara mkono unanigusa begani wa yule dingi huku akisema kwa sauti ya chini sana "dogo nisaidie paper imeniona". Namjibu "hata mimi ngoma ngumu". Tunaendelea na mtihani baada ya kama dk6 ananigusa tena huku akisema "nipe tu majibu hayo hayo" .Unajua nini kilichofuatia ?! WOTE MIMI NA MZEE WANGU TULIKUTANA KWENYE SUPP.
 
Nikiwa mwaka wa kwanza nilikuwa navuta sana bangi sasa kuna dada mmoja wa kizanzibar alikua ananiona kama shetani vile hata kugonganisha macho na mm hataki ila bahati yake mbaya kwenye pepa tunakaa jirani, cku moja pepa imempiga akanishtua na mm bila hiyana nikamuwekea akawa anakopy tu kuanzia siku ile akaanza shobo siku zimeenda akawa ananitafuta hadi ucku kusoma wote baadae akawa akiona nimezubaa ananipa buku mbili nikanunue ganja ili tukae wote, kupitia yule dada nikajua hawa wavaa hijabu ni washenz kuliko hata hawa vicheche!
 
Haaa haaa haaa dah nakumbuka mengi na nilipitia mengi mnoo nikikumbuka nilikua naenda club toka jumanne had jumapili huku nimejioza mwee. Na sup sirudi.watu walikua hawaelewi inakuaje ila nilitoka na Hon ya 4.1 hapo ndo ujue Muache Mungu aitwe Mungu.. Kwetu nikirudi mpole kumbe nimenusurika fukuzwa chuo kwa fujo.. Dodoma sitakusahau kamwe...
 
Hilo sio wazo lako ,bali la mwandishi wa kitabu wewe umekariri tu

Hivi kwanini elimu yetu hairuhusu free thoughts?
Ukipata majibu ya swali lako fanya mpango uandike kitabu tukisome. Tutakifanya kama reference.
Au sio mzee baba?
 
AISEE kwanza namshukuru jakaya kwa ile kozi kutupa full sponsor ya kutoka wizara ya nishati na madini maana bila hivyo cjui kama ningemaliza maana ilikuwa na module jiwe zilizoshiba naizungumzia petroleum geoscience

Picha linaanza ni UE ya mwaka wa pili ratiba imetoka paleontology ya Dr mishra imewekwa siku moja na support ya physics dah Cr kumwambia aende akabadilishe ratiba department kachelewa dah mungu mwenye anajua tulipiga paleontology asubuhi mchana physics yaani kila ukitisa kichwa desa za paleontology haziondoki kichwani ikabidi nimcheck msimamizi na kumwambia ukweli dah jamaa akaniombea booklet ya kupigia chabo kwa mshikaji wa geology dah mwisho wa siku nikapata B
Ila cha moto nilikiona siku hiyo.
 
Back
Top Bottom