Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,111
- 34,943
--- UNAKUBALI AU UNAKATAA, JE WAJUA KUWA...!? ---
1. MASIKINI akitembea kwa miguu, kwake ni shida na kutokuwa na usafiri ni mateso, Ila kwa Tajiri Kutembea kwa miguu ni mazoezi tu na ni tiba kuondoa Msongo wa mawazo au STRESS.2. Maneno mazuri yenye hekima kutoka kwa MASIKINI yataitwa kimbelembele na makelele au kutaka kujionyesha, yakisemwa na TAJIRI yataitwa Maneno yenye BUSARA!
3. MASIKINI akizaa au akiwa na mtoto mmoja au wawili tu, ataambiwa ni laana na hana kizazi au ni kwa sababu anaogopa GHARAMA za maisha, ila TAJIRI akiwa na mtoto mmoja au wawili ni uzazi wa mpango na usomi.
4. MASIKINI akila Dagaa (dagaa mchele) au Kisamvu kwa maskini ni mlo wa kawaida na ni dalili ya kutokuwa na pesa na ni shida zimesababisha. Ila kwa TAJIRI ni chakula cha kujenga mwili.
5. Binti wa KIKE wa maskini akivaa nusu uchi ataitwa MALAYA/CHANGU DOA tena hana ADABU, ila wa TAJIRI ataitwa Miss Fulani au Modo au yupo Kisasa zaidi anakwenda na wakati...
6. MASIKINI akiwa na MARAFIKI wachache wa karibu, ataitwa mchoyo kama sio mchawi, ndio maana hana marafiki, ila kwa TAJIRI kuwa na marafiki wachache ndio usasa na kwenda na wakati na wataitwa washauri wa Kibiashara.
7. MASIKINI akihalikwa kwenda kwa TAJIRI ataambiwa anajipendekeza, ila kwa TAJIRI kwenda kwa masikini ataambiwa anajali na ni mpenda watu.
8. SIKU masikini akivaa za MTUMBANI au nguo mpya na akipendeza, ataambiwa anajionyesha, ila TAJIRI akivaa mpya na hata kama ajapendeza, itaitwa fasheni tu hiyo.
9. MASIKINI siku akipata KIPATO kizuri, watu watasema ni NGEKEWA tu hiyo, au utasikia wakisema aaah! Kenda kwa BIBI/BABU kuroga, Ila TAJIRI akipata zaidi, watasema KAJAALIWA kipato.
10. MASIKINI akipata MARADHI na yakamuondoa duniani, hata kama ni Malaria, watu watanong'ona tu kuwa ni UKIMWI tena akiugua muda mrefu, ila tajri akifa kwa UKIMWI au NGOMA tena kwa muda mrefu watasema kuwa ni SHINIKIZO la Damu tu... Yaani presha au kauguwa ghafla tu au Kaugua Muda mfupi!
11. MASIKINI akifa, utasikia wakisema aah! Alikuwa mwingi naeee! Ndio maana hakuacha chochote, hata kama alikuwa na mke na watoto, na nyumba kule Manzese kwa mfuga Mbwa, ila TAJIRI akifa utasikia, amewacha Mke na watoto na PENGO lake halita zibika.
---JE UNAKUBALI AU UNAKATAA...!?---