Unajua umuhimu wa msamaha?

Unajua umuhimu wa msamaha?

Joined
Feb 9, 2014
Posts
20
Reaction score
6
KWA muda mrefu nimekuwa nikipata maswali kutoka wadau na wengine wakieleza matatizo waliyonayo katika uhusiano na wapenzi wao. Kati yao, wapo ambao wanateswa na jambo dogo sana; ni dogo lakini linawashinda kiasi sasa limekuwa kubwa!
Msamaha. Katika uhusiano ni vyema kukubali kwamba, mwenzako si mkamilifu na anaweza kukosea, hivyo ana wajibu wa kuomba msamaha lakini pia nawe unapaswa kupokea msamaha wa mwenzako hasa kama ameomba kwa dhati. Ukiacha kusamehe na kubaki na kinyongo, utabaki na maumivu makali moyoni mwako.
Ni maumivu hayo ndiyo yatakayoweza kusababisha matatizo mengine katika uhusiano wako. Kubali kusamehe, omba msamaha kwa mwenzako, mara nyingi inavyowezekana ili uhusiano wenu uendelee kuwa wenye amani. Acha kuweka vinyongo moyoni mwako.
Ahsanteni sana. Naamini dondoo imeeleweka vizuri.
- Joseph Shaluwa.
 
Ni kweli kabisa,na hivi sipendi makuu..naweza hata kupiga magoti
 
Joseph Shaluwa ni yule anaandikaga makala kwenye magazeti ya Global!!!!!!!

asante kwa dondoo
 
Joseph Shaluwa ni yule anaandikaga makala kwenye magazeti ya Global!!!!!!!

asante kwa dondoo

kumbe na weye unamjua..me huwa nasoma article zake siku zote nzuri sana...
JOSEPH SHALUWA ndo wewe au siee?am a big fan of ur writings
 
Last edited by a moderator:
kuomba msamaha na kusamehe ni jambo jema lkn kutenda kosa hilo hilo kila wakati na kuomba msamaha kunachukuliwaje na mtoa msahama?
 
Ni jambo jema kusameheana lkn kwa bahati mbaya walio wengi huuchezea sana msamaha . Mara nyingi kwenye mahusiano au ndoa mambo magumu sana kusameheana ni kukosa uaminifu na wengine huona kuwa kusamehewa ni haki yao hivyo kila wakikosea huomba msamaha kiasi kwamba hata neno msamaha hupungua uzito.

Naamini msamaha hupunguza wingi wa maradhi na huleta afya kwa mtoa msamaha . Msamaha una maana tu pale mtu atakapojua kosa lake na kuamua kuacha au kujifunza kuacha. Kuna majeraha ambayo husababishwa na tukio hata mtu kama akitoa msamaha bado atahitaji uponyaji wa majeraha hayo. Majeraha yaweza chukua muda mrefu kupona na mara nyingine unaweza ukashindwa kuyatenganisha na msamaha. Wengi huhisi hawajasamehe hasa waonapo majeraha bado yamo mioyoni mwao ingawa kiuhalisia huwa tayari wamesamehe.

Nafikiri itakua vema kuepuka kama itawezekana kufanya makosa ya makusudi kwenye mahusiano. Kama nilivyoeleza hapo juu waweza sababisha madhara makubwa kwa mwenzako na kama mtapendana kwa dhati na kutoacha mlango wazi au kuwafungulia mlango wenu wengine lazima mtaishi kwa amani na majeraha free.
 
naomba kukuliza kaka shaluwa! je ww unayajua saan mapenzi au! maan naona makala zako nyiingi znahusu mapenzi!
 
Msamaha ni jambo la kher endapo mwombaj wa msamaha anamaanisha na kutorudia kosa pia anaesamehe na asamehe kwel bila kuwa na kinyongo
 
haya kaingia POST ya kwanza na style yake humu JF tofauti na ya akina CHAI CHUNGU au Mzizi mkavu
tusubirie mengi km ya huko Global
 
KWA muda mrefu nimekuwa nikipata maswali kutoka wadau na wengine wakieleza matatizo waliyonayo katika uhusiano na wapenzi wao. Kati yao, wapo ambao wanateswa na jambo dogo sana; ni dogo lakini linawashinda kiasi sasa limekuwa kubwa!
Msamaha. Katika uhusiano ni vyema kukubali kwamba, mwenzako si mkamilifu na anaweza kukosea, hivyo ana wajibu wa kuomba msamaha lakini pia nawe unapaswa kupokea msamaha wa mwenzako hasa kama ameomba kwa dhati. Ukiacha kusamehe na kubaki na kinyongo, utabaki na maumivu makali moyoni mwako.
Ni maumivu hayo ndiyo yatakayoweza kusababisha matatizo mengine katika uhusiano wako. Kubali kusamehe, omba msamaha kwa mwenzako, mara nyingi inavyowezekana ili uhusiano wenu uendelee kuwa wenye amani. Acha kuweka vinyongo moyoni mwako.
Ahsanteni sana. Naamini dondoo imeeleweka vizuri.
- Joseph Shaluwa.

yale magazeti yatahamia humu
 
Dedication:nimekusamehe mpenzi by ....
 
MARAFIKI ZANGU,
Ni kweli, mimi ndiye JOSEPH SHALUWA ninayeandikia kwenye magazeti ya Global Publishers na vitabu mbalimbali. Nimeamua kutumia jina langu halisi na nitakuwa tayari kubadilishana mawazo na marafiki humu JF.
Mkijisikia kuniuliza maswali, nipo tayari kuyajibu kwa kadiri nafasi ya muda wangu itakavyokuwa ikiniruhusu. Aidha, kuanzia leo, kila siku nitawaletea simulizi yangu ya MKATABA WA SIRI.
Ahsanteni sana.
Karibuni kwa burudani zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom