GE2025 Unajua nini kuhusu Dr. Emmanuel John Nchimbi?

GE2025 Unajua nini kuhusu Dr. Emmanuel John Nchimbi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mbinafsi sana anarud jimboni kwake wakati wakuomba kura tu, baada ya hapo nyumba yaota nyasi
 
Team Lowassa lia lia,mwanamtandao ambae hakuwahi kuasi .Ni mmiliki wa account ya Kigogo twitter.Yaani ndoto yake ni kuwa Rais bila kutoa Jasho kama ilivyokuwa kwa Samia.Inshort Samia hatomaliza term ya pili.I wish this time jeshi liingilie kati .
Kivipi atapenya? SSH atakuwa wap muda huo?
 
Team Lowassa lia lia,mwanamtandao ambae hakuwahi kuasi .Ni mmiliki wa account ya Kigogo twitter.Yaani ndoto yake ni kuwa Rais bila kutoa Jasho kama ilivyokuwa kwa Samia.Inshort Samia hatomaliza term ya pili.I wish this time jeshi liingilie kati .
Rafiki WA Mkuu WA idara pendwa ,wamekua wote Kwa Pele
 
Team Lowassa lia lia,mwanamtandao ambae hakuwahi kuasi .Ni mmiliki wa account ya Kigogo twitter.Yaani ndoto yake ni kuwa Rais bila kutoa Jasho kama ilivyokuwa kwa Samia.Inshort Samia hatomaliza term ya pili.I wish this time jeshi liingilie kati .
Kigogo tweeter fuatilia vizuri. Nchimbi ni mtu mwenye msimamo sana sijui amekuja kuaje kukubali kua Makamu wa Rais bila kufuata taratibu JK mjanja sana alijua Nchimbi atasumbua chap Makamu
 
Rafiki WA Mkuu WA idara pendwa ,wamekua wote Kwa Pele
Yes Nchimbi idara kitambo na mtu mwenye msimamo sana sijui ilikuaje akakubali kua makamu bila kufuata taratibu na ni mtu anaekijua chama pia vizuri. Nchimbi ni mtu msimamo anaemchukulia poa Nchimbi ni wakumuonea huruma yeye ndo alietoka nje wakati wamemkata Lowassa na kusema CCM haijafuata taratibu mbele ya kina Mkapa na JK nafikiri alipewa Umakamu asimsumbue
 
Acha uongo.Huyo mtu wa Songea huko hata kama alizaliwa mkoa mwingine.Ila huyo ni mngoni.
Kazaliwa Mbeya kakulia Dar baba ake alikua RPC Mtwara
Kasoma
primary Oysterbay
O level Uru na Sangu Mbeya
A level Forest Hill Mbeya
Chuo IDM Mzumbe

Mtoto wa mjini haswa
Mngoni mpe pesa atafikisha ....
 
Inaonekana taarifa zake zinatofautiana. Nyingine hii hapa:

Dk Emmanuel Nchimbi alizaliwa Desemba 24, 1971 mkoani Mbeya, (atafikisha miaka 44 Desemba mwaka huu). Elimu yake ya Msingi aliianzia jijini Dar es Salaam katika Shule ya Msingi Oysterbay kati ya mwaka 1980 – 1986.

Baba yake mzazi, Mzee John Nchimbi kutoka wilayani Songea ni askari mstaafu wa Jeshi la Polisi na wakati anastaafu alikuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara. Mzee Nchimbi pia amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kwa vipindi viwili kupitia kundi la majeshi na baadaye katibu wa CCM wa mkoa, alikoma kushiriki masuala ya kisiasa mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.

Dk Nchimbi alijiunga na elimu ya sekondari kwenye Shule ya Sekondari Uru kati ya mwaka 1987 – 1989 (kidato cha I – III) halafu akahamia Shule ya Sekondari Sangu na kukamilisha kidato cha nne mwaka 1989 – 1990.

Nchimbi alisoma Shule ya Sekondari ya Forest Hill, Mbeya masomo ya kidato cha V na VI mwaka 1991 – 1993. Alijiunga katika Chuo cha IDM Mzumbe (Morogoro) na kuhitimu Stashahada ya Juu ya Utawala (mwaka 1994 – 1997).

Wakati anahitimu IDM, pia alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na mwaka uliofuatia (1998), alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Dk Nchimbi amewahi kuajiriwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kati ya mwaka 1998 – 2003.

Alisoma shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2001 – 2003 akibobea kwenye maeneo ya (benki na fedha).

Dk Nchimbi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda (mwaka 2003 – 2005) na (mwaka 2008 – 2011) alisoma na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Dk Nchimbi amemuoa Jane na wana watoto watatu.

Mbio za ubunge

Dk Nchimbi alirudi nyumbani kwao (Songea Mjini) kuanza harakati za ubunge tangu alipokuwa anaongoza UVCCM. Ilipotimu mwaka 2005, aliingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi akakutana na Edson Mbogoro wa Chadema aliyekuwa mpinzani wake mkuu. Dk Nchimbi alisaidiwa na mtandao mkubwa wa CCM na kupata ushindi wa asilimia 67.6 dhidi ya asilimia 30.5 za Mbogoro.

Mara tu baada ya kuwa mbunge, Rais Kikwete alimteua kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, hii ilikuwa Januari 2006, alidumu kwenye wizara hiyo hadi Oktoba 2006 alipohamishiwa kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana – hapa pia alikuwa Naibu Waziri tangu Oktoba 2006 hadi Februari 2008 kisha Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa ambako pia alikuwa Naibu Waziri hadi Novemba 2010.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Nchimbi alijitosa tena Jimbo la Songea Mjini. Kampeni za 2010 zilimnyima usingizi pamoja na kuwa chama chake kilikuwa kimechukua asilimia zaidi ya 90 ya vijiji, vitongoji na mitaa mwaka 2009.

Kama kawaida, alipambana tena na Mbogoro wa Chadema na kumshinda kwa mara ya pili, japo safari hii Dk Nchimbi akipoteza takriban ushindi wa asilimia 10 ukilinganisha na mwaka 2005. Katika uchaguzi huo, alipata asilimia 59.9 dhidi ya 37.48 za Mbogoro.

Upandaji vyeo wa Nchimbi uliendelea, Rais Kikwete alimpa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo akiwa Waziri kamili, alidumu hapo hadi Mei 2012 alipohamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani kabla ya kujiuzulu Desemba 2013.
Form v na vi alisoma Foresthill ya Morogoro sio Mbeya.
 
Dr. Emmanuel Nchimbi amewahi kushika nafasi mbalimbali za ajira na uongozi, nyingi zikiwa ndani ya serikali na chama. Mpangilio wake wa kazi unaweza kuonekana hivi:

Ajira na Nafasi Alizoshika

1. Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini – (2005–2015)

Alichaguliwa kupitia CCM na kushiriki kikamilifu katika mijadala na kamati za Bunge.

2. Naibu Waziri katika wizara kadhaa (2006–2010)

Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana

Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana

Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

3. Waziri
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana (2010)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (2012–2013)
4. Balozi wa Tanzania

Brazil (2016–2021)

Misri (2022–2023)
5. Katibu Mkuu wa CCM – kuanzia Januari 2024 hadi sasa.
6. Mgombea Mwenza wa Rais (2025)
Ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kugombea nafasi ya Makamu wa Rais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Rais wa Tanzania 2026!
 
Team Lowassa lia lia,mwanamtandao ambae hakuwahi kuasi .Ni mmiliki wa account ya Kigogo twitter.Yaani ndoto yake ni kuwa Rais bila kutoa Jasho kama ilivyokuwa kwa Samia.Inshort Samia hatomaliza term ya pili.I wish this time jeshi liingilie kati .
Mara asemwe februari ndo kigogo.. Nawe umekuja na hii ya john
 
Back
Top Bottom